Maendeleo Bank pamoja na wewe. Bank ya Maendeleo leo imezindua promosheni iitwayo Maendeleo pamoja na wewe. Akizungumza kwenye hafla hiyo Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank Ibrahim Mwangalaba alisema “ Leo tumekutana hapa kwa ajili ya tukio fupi tu la kuzindua rasmi promosheni tuliyoipa jina la Maendeleo Bank pamoja na wewe”.
Aliongeza kusema “Promosheni ya Maendeleo Bank pamoja na wewe ni mahususi kwa wateja waliopo au wapya. Kama mnavyojua Maendeleo Bank imeanzishwa miaka 4 iliyopita na imepiga hatua kubwa sana; Tumeongeza matawi kutoka moja hadi 3 ambayo ni Luther House, Mwenge na Kariakoo, tumebuni bidhaa nyingi, tumepata faida nzuri katika kipindi kifupi hadi kufikia Milioni 550, Amana za benki zimeongezeka hadi kufikia Bilioni 34,tumetoa mikopo inayofikia Bilioni 27 tumeajiri wafanyakazi 63, na kama tutaruhusiwa na CMSA tunatarajia kukaribisha wanahisa wapya kupitia Soko la awali yaani IPO hivyo kukuza wigo wa umiliki wa benki na mtaji wa kufanya mambo mengi zaidi”.
Alimalizia kwa kusema , Sisi kama benki yenye kulenga kuwapa wateja wetu Maendeleo tunawapa wateja watakaofungua akaunti za akiba au timiza nafasi yakujishindia ; Viwanja, tani za cement, mabati au ada za shule kwa wale watakao fungua au kuweka amana kwenye Maendeleo Junior.
Promosheni hii ni ya miezi 3.
No comments:
Post a Comment