Mama salma akimkabidhi Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan mpango mkakati wa TGGA
Samia Suluhu Hasan akimkabidhi Mlezi mstaafu wa TGGA zawadi ya saa aliyopewa zawadi na uongozi wa TGGA kwa ajili ya kumbukumbu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Abraham Ntambara.
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya
Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan amewataka wasichana ambo ni wanachama wa chama
cha Tanzania Girl Guides Association (TGGA) kuzingatia mafunzo wanayopatiwa kwa
ajili ya maisha yao ya baadaye.
Kauli hiyo aliitoa leo jijini Dar es Salaam wakati
akikabidhiwa kijiti cha kuwa mlezi wa chama hicho kutoka kwa Mama Salma Kikwete
anayesitaafu nafasi hiyo aliyoihudumu kwa zaidi ya miaka 12.
“Niwatake tu watoto wangu kutochukulia kwa mzaha mafunzo
mnayopatiwa kwani ni tija kwa maendeleo ya Taifa,” alisema Makamu wa Rais.
Aidha aliwaahidi wanachama kutowaangusha katika kutekeleza
majukumu ya kukilea chama hicho ambapo alimpongeza Mama Salma Kikwete kwa
kuweza kukiongoza vizuri kwa mafanikio makubwa licha ya kuwa na majukumu
mengine.
Aliahidi kuifanyia changamoto iliyotajwa ya matumizi ya
mitandao ya kijamii ambapo alisema atalisimamia hilo kwani ni vizuri kutumia
mitandao hiyo kwa kuzingatia maadili kutokana na hivi sasa watu kuitumia
vibaya.
Pia alitoa pendekezo la chama hicho kubuni miradi mingine
ambayo inaweza kuwaingizia fedha ili kuacha kutegemea wahisani.
Mama Salma Kikwete wakati akimuachia jukumu hilo la kukilea
chama hicho alimkabidhi vitu vitatu ambavyo ni Bendera ya Taifa ya chama,
Katiba na mpango mkakati wa chama na kumvalisha Skafu ya chama kama ishara ya
kukabidhiwa rasmi kijiti hicho.
Aidha alisema kuwa chama kimekuwa na mafanikio makubwa ikiwa
ni pamoja na kuweza kuongeza wanachama kutoka 97,143 hadi kufikia wanachama 100,008
mwaka huu.
Aliongeza kwamba wanatarajia mwezi Septemba kuapisha
wanachama 300 katika mkoa huku akieleza kwamba tayari wamekwisha sajili zaidi
ya wanachama 2000 katika mkoa wa lindi.
Kikundi cha sanaa cha Ilala kikitumbuiza
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, ambaye pia ni Kamishna wa TGGA, Sophia Mjema akimlaki aliyekuwa Mlezi wa TGGA Mama Salma Kikwete
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna Mkuu wa TGGA, Symphorosa Hangi
Salma Kikwete akisalimiana na Katibu Mkuu wa TGGA, Grace Shaba
Mama Salma Kikwete akisalimiana na Kamishna wa TGGA
Samia akiangalia kazi mbalimbali zinazofanywa na Girl Guides
Samia akipata maelezo kutoka kwa Mkufunzi wa Girl Guides Ruth kuhusu kazi mbalimbali za TGGA
Samia na Salma Kikwete wakilakiwa na Girl Guides
Brass Band ya Polisi ikiongoza wimbo wa Taifa
Viongozi mbalimbali wakiwa katika sherehe hiyo
Baadhi ya makamishna wa TGGA wakiwa katika sherehe hiyo
Mwenyekiti wa TGGA Profesa Martha Qorro akitambulisha baadhi ya wageni waalikwa
Kamishna Mkuu wa TGGA Symphorosa Hangi akisema neno la utangulizi pamoja na kutambulisha wageni waalikwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya TGGA, Anna Abdalah akihutubia wakati wa sherehe hiyo
Aliyekuwa Mlezi wa TGGA, Mama Salma Kikwete akihutubia kabla ya kumkabidhi ulezi Makamu wa Rais Samia
Ni furaha iliyoje
Salma Kikwete akimvisha skavu Mlezi mpya wa TGGA, Samia Suluhu Hassan
Wasanii wa Shule ya Msingi Umoja wakitumbuiza wakati wa sherehe hiyo |
Ni wakati wa furaha |
Mkuu wa Wilaya ya Ilala, Mjema na Mwenyekiti wa Bodi ya TGGA, Anna Abdalah wakichenza ngoma |
Mama Samia akimtunza fedha kiongozi wa kikundi cha Umoja kwa kucheza vizuri
Kamishna Mkuu wa TGGA akimkabidhi zawadi ya saa Mlezi mstaafu wa TGGA, Mama Salma Kikwete
Mama Salma akionesha Saa hiyo
Girl Guides wakighani shairi maalumu
Baadhi ya makamishna wakiimba wimbo maalumu
NI FURAHA TELE
Viongozi na makamishna wakiwa katika picha ya pamoja na Mlezi mpya wa TGGA, Samia
Mlezi mpya, Mama Samia akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi na makamishna wa mikoa
Mama Samia na Salma Kikwete wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wa TGGA
Girl Guides wakiwa na Mama Salma Kikwete pamoja na Mlezi mpya, Samia
No comments:
Post a Comment