Advertisements

Thursday, July 20, 2017

Marehemu Jaji Upendo Msuya kuzikwa Jumamosi

Mwili wa aliyekuwa Jaji wa mahakama kuu ambaye amejiuzulu hivi karibuni, Upendo Msuya unatarajiwa kuzikwa Jumamosi katika makaburi ya Kinondoni saa 9 mchana.
Jaji Msuya alifariki Jana katika hospitali ya Kairuki alipokuwa amelazwa akiugua ugonjwa wa Kiharusi.
Msemaji wa familia ambaye pia ni mume wa marehemu Mhandisi Hilary Msuya amesema misa ya kumuaga marehemu itafanyika Kanisa la KKKT Wazo Jumamosi asubuhi
"Jumamosi asubuhi tutafanya ibada fupi hapa nyumbani na baadaye tutaelekea kanisani kwa ajili ya misa"amesema

No comments: