Advertisements

Sunday, July 2, 2017

Mchakato wa uchaguzi wa TFF wasimamsishwa

Mwenyekiti wa Kamati ya uchaguzi mkuu wa TFF Revocatus Kuuli amesitisha mchakato mzima wa uchaguzi hadi hapo utakapotangazwa tena baadae.
Kuuli ametangaza uamuzi huo mbele ya waandishi wa habari katika ofisi za TTF mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kamati ya uchaguzi.
“Kikao chetu cha leo kimefanyika lakini hakijatoa maamuzi ya matatizo yaliyotokea jana.”
“Mimi kama Mwenyekiti wa Kamati nimechukua maamuzi ya dhamana niliyonayo, nimemuandikia Katibu juu ya dhamira yangu kuangalia upya mwenendo mzima wa kamati. Wamekubaliana na maombi yangu na wamenipa barua kwamba wanaona sahihi mchakato mzima usimame mpaka matatizo yaliyotokea yatakapo pelekwa kwenye kamati ya utendaji ambayo ndio yenye mamlaka ya mwisho.”
“Wamesema wataitisha kikao Julai 4, 2017. Matatizo yalikua mengi, kuna watu wamekatakatwa majina kwa uonevu tu, taratibu zinataka kupindishwa kwa sababu ya kutaka kupendelea watu fulani.”
“Mimi siwezi kuwa sehemu ya kamati ambayo ipo namna hii, kwa hiyo nashukuru barua yangu imepokelewa na imefanyiwa kazi kama nilivyokuwa nimetaraji.”
Julai 4, 2017 utatolewa uamuzi kama uchaguzi utaendelea au vinginevyo baada ya kamati ya utendaji ya TFF kukaa na kuamua.

No comments: