Advertisements

Friday, July 14, 2017

Mhe. Makame Mbarawa afanya ziara JNIA

 Mkuu wa Kitengo cha Idara ya Uhamiaji Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere, Bw. Flugence Andrew (kulia) akitoa maelezo ya utaratibu unaotumika kulipia viza kwa Mhe. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano leo alipofanya ziara kwenye jengo la abiria la kiwanja hicho. 
 Afisa wa Benki ya NMB, Bi. Leah Rutayungurwa  (aliyendani ya dirisha) leo akimmsikiliza Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof Makame Mbarawa aliyetaka kujua muda anaohudumiwa abiria mmoja wakati akilipia viza kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA).
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa leo akiwa katika mfumo wa kupokelea mizigo kwa abiria wanaowasili kwenye Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere alipofanya ziara ya kutembelea maeneo mbalimbali. Mwenye kizibao ni Kaimu Mkurugenzi wa kiwanja hicho, Bw. Joseph Nyahende.
Mhe. Prof. Makame Mbarawa, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (TBII-JNIA), mwenye kizibao akielezea jambo katika meza ya ukaguzi wa tiketi za abiria wanaosafiri. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA), Bw. Salim Msangi.
 Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Mhe. Prof. Makame Mbarawa (kulia) akifurahia jambo na Waziri wa Fedha na Mipango, Mhe. Phillip Mpango (kushoto)  na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Dkt. Susan Kolimba na Katibu Mkuu  sekta ya Uchukuzi Dkt. Leonard Chamuriho (mwenye mkoba mweusi) leo walipokutana kwenye Jengo la Watu Mashuhuri la Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere.

1 comment:

Anonymous said...

Hakika bureaucracy ilipo kwenye uwanja wa ndege wa JNIA katika kushughulikia Visa ni janga linalotoa taswira mbaya ya nchi.Hatua za haraka zinahitajika kuondoa hii aibu.