ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, July 1, 2017

MOBISOL YAZINDUA TV YA SOLA YENYE UWEZO WA KUENDESHA VIFAA VINGINE

Mkuu wa Masoko na Uhusiano wa kampuni ya Mobisol, Leslie Katharina Otto, (kushoto)akitoa maelezo kwa mmoja wa wateja waliotembelea kwenye banda la Mobisol kwenye maonyesho ya kimataifa ya biashara yanayoendelea jijini Dar es salaam.
Kaimu Balozi wa Ujereumani hapa nchini John Reyels (kushoto) akimsikiliza kwa makini Afisa Mtendaji Mkuu wa Mobisol Afrika Mashariki, Henrik Axelsson Lilja , wakati wa uzinduzi wa kutoa huduma za Mobisol jijini Dar es Salaam, kwenye banda la Ujerumani lililopo kwenye Maonyesho ya 41 ya Biashara ya Kimataifa maarufu Sabasaba jijini Dar es Salaam .

Ofisa Mkuu wa Kampuni ya Mobisol Afrika Mshariki, Henrik Axelsson Lilja, akionyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) moja ya TV ya Sola
Mwakilishi wa Mobisol kanda ya Dar es Salaam, Allan Rwechungura akiongea na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa kampuni Mobisol mkoani Dar e salaam na Sola Tv kwenye banda la maonyesho la kampuni hiyo lililopo uwanja wa SabaSaba ---Kampuni ya Mobisol kutoka nchini Ujerumani ambayo inafunga na kuuza vifaa bora vya nishati ya umeme imezindua bidhaa mpya ya kipekee kwenye soko la Tanzania, ambayo ni TV ya sola inayojitegemea kabisa.
Akiongea jijini Dar es Salaam wakati wa Uzinduzi wake, kwenye banda la Ujerumani, katika viwanja vya sabasaba, Meneja Mkuu wa Mobisol Afrika Mashariki, Henrik Axelsson akiwa na mwakilishi wa Mobisol, kanda ya Dar es salaam, Allan Rwechungura, amesema TV hii mpya ya kioo bapa yenye ubora wa hali ya juu ya sola inajitegemea na inauwezo wa kuwasha taa na kuchaji simu hivyo ni ya kipekee na inajitegemea kwa upande wa nishati.
TV hii kisasa ya kioo bapa yenye ubora wa hali ya juu, ina betri inayofanya kazi hadi masaa 10, ina uwezo wa kuwasha taa, una waranti ya miaka 3 na huduma (service) baadaa ya mauzo.
Alisema katika msimu huu wa Sabasaba kampuni ya Mobisol imetoa punguzo maalumu kwa ajili ya kuwawezesha watanzania wengi kuunganishwa na umeme wa sola wa uhakika ikiwemo kujipatia vifaa imara na vya kisasa vilivyotengenezwa kwa teknolojia ya Kijerumani kwa gharama nafuu na kuweza kulipia kwa awamu mpaka kufikia kipindi cha miaka mitatu.
”Ofa hii inawezesha wateja wetu watakaolipa fedha taslimu kuunganishwa na mtandao wa Mobisol kupata punguzo hadi asilimia 25% na watakaolipia kwa awamu gharama ya kuanzia ni shilingi 59,000/- ambapo makato ya kila mwezi itakuwa shilingi 33,500/- ambapo kwa miaka 3 itakuwa kiasi cha shilingi 1,266,000/-”. Alisema Rwechungura.
Hii ni fursa ya kuwapatia zawadi ya maendeleo familia yako na wale uwapendao kijijini! Aliongeza kuwa kampuni ya Mobisol ambayo sasa imeanza kutoa huduma zake hapa jijini Dar es Salaam, ina mitambo ya nguvu ya kwa ajili ya matumizi mbalimbali ya nyumbani ya wati 80, 120, na 200 mbayo inakuja pamoja na betri, taa, TV, redio, tochi na waya ya kuchaji simu. Hivyo kumwezesha mtu anayeishi eneo ambalo umeme haujafika kutokuwa na tofauti na mtu aishiye mjini.
Akibainisha zaidi uwezo wa kufanya kazi wa TV hii ya sola inayojitegemea ikitumika kwa TV, kuwasha taa 3 (za Wati 1) kwa muda wa masaa 6 na kuchaji simu 2 unaweza kufanya kazi kati ya masaa 6 hadi 9. Matumizi ya King’amuzi na kuwasha taa 3 kwa masaa 6 ya kuchaji simu 2 unaweza kufanya kazi kati ya masaa 5 na 7.
Rwechungura aliendelea kufafanua kuwa iwapo mteja atawasha TV kwa masaa 4 na kuchaji simu 2 ataweza kutumia taa kwa masaa 10 hadi 15.
“Mtambo huu wa Tv ya sola unaowezesha matumizi ya aina mbalimbali unapatikana kwa gharama ya shilingi 950,000 na vifaa vya umeme ambayo mteja ataweza kununua na kutumia kwenye mtambo huu ni seti ya taa ya umeme yenye 1W au 2W, kifurushi cha King’amuzi cha Zuku chenye chaneli za kulipia, Redio ndogo na seti ya kuchaji simu. Hii ni fursa nyingine ya pekee kwa wateja kujiunga na familia ya Mobisol na kufurahia maisha ya kisasa kwa kutumia vifaa vya teknolojia bora kutoka Ujerumani” Alisema.
Mobisol ni kampuni pekee katika kanda ya Afrika yenye mitambo ya kuzalisha umeme wa nishati ya jua wenye nguvu na inauza vifaa bora vya majumbani vya matumizi ya nishati ya umeme wa jua ambapo pia imekuwa inatekeleza mpango wa kusambaza nishati ya umeme wa jua kwa kulipia kwa awamu. Kufikia sasa inao mtandao wa wateja zaidi ya 62,000 nchini Tanzania na zaidi ya wateja 85,000 katika kanda ya nchi za Afrika Mashariki.
Mobisol sasa ipo katika mikoa 23 nchini Tanzania na inaendelea kusogeza huduma karibu na wahitaji.

No comments: