Advertisements

Tuesday, July 25, 2017

OFISI YA MAKAMU WA RAIS YAANDAA WARSHA YA MAFUNZO YA KEMIKALI NA TAKA HATARISHI KWA MAZINGIRA KWA MAAFISA SHERIA, MAAFISA FORODHA NA WAKAGUZI WA MAZINGIRA NA UBORA WA BIDHAA.

Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bwana Clifford Tandari amesisitiza kuwa ni muhimu kujenga uelewa kwa Maafisa Sheria, Maafisa forodha na wakaguzi wa mazingira na ubora wa viwango Nchini ili waweze kutambua kemikali na taka hatarishi kwa mazingira na matumizi ya Binadamu. Ameyasema hayo mjini Morogoro wakati wa ufunguzi wa Warsha ya siku tatu iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.

Aliongeza kuwa moja ya changamoto ambayo dunia inaikabili kwa sasa ni usimamizi wa kemikali na taka hatarishi katika jamii zetu. " Hizi kemikali na taka zinahitajika kusimamiwa vizuri ili kupunguza madhara ya afya kwa binadamu na mazingira na pia Wanawake na watoto wapo kwenye hatari kubwa ya kuathirika na kemikali hizo na kupeleka magonjwa makubwa hatarishi yatokanayo na kemikali hizo" alisema.

Bwana Tandari aliwataka Maofisa walioalikwa kujengewa uelewa wa kemikali na taka hatarishi wakaitumie elimu hiyo katika majukumu ya kazi zao za kila siku na hivyo kupelekea usimamizi stahiki wa wa taka na kemikali hizo. Na hiyo itapelekea kupunguza na kumaliza kabisa athari za kemikali na taka hatarishi katika Nchi yetu.

Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais - Idara ya Mazingira ili kuwajengea uelewa Maafisa hao ili kuweza kudhibiti uingizwaji na usambazaji wa kemikali hizo hatarishi Nchini. Katika Warsha hiyo Maafisa wa forodha, sheria na wakaguzi wa Mazingira na viwango vya ubora wamehudhuria hivyo basi uelewa juu ya kemikali hizo utaongezeka na utawasaidia katika majukumu yao ya kila siku wanapokua makazini.
Mkurugenzi wa Idara ya Mazingira -Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi akimkaribisha Mgeni Rasmi kufungua warsha ya mafunzo ya kemikali na taka hatarishi kwa mazingira kwa Maafsa sheria na maafisa Forodha. Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais inafanyika mjini Morogoro.
Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Bwana Clifford Tandari akifungua Warsha ya mafunzo ya kemikali na taka hatarishi kwa mazingira kwa Maafisa Sheria pamoja na Maafsa Forodha na Wakaguzi wa mazingira na ubora wa bidhaa . Warsha hiyo imeandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais.
Sehemu ya Wadau waliohudhuria warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais juu ya kujenga uelewa kwa Maafisa Sheria, Maafisa forodha na Wakaguzi wa mazingira na ubora wa bidhaa kutoka Taasisi za Serikali
Mgeni Rasmi ambaye ni Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Warsha hiyo iliyoandaliwa na Ofisi ya Makamu wa Rais inayofanyika mjini Morogoro.
Mmojawapo wa watoa Mada katika warsha hiyo Bwana Faraja Ngerageza kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais akiwasilisha mada.
Mgeni Rasmi katika warsha hiyo Bwana Clifford Tandari pamoja na Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais Bwana Richard Muyungi (kulia) wakimsikiliza Mwakilishi wa WWF Africa Bwana Patrick Chibada wakati wa Warsha hiyo.

No comments: