Advertisements

Sunday, July 16, 2017

PAMOJA NA REFA KUIBEBA NEW YORK, YAKUBALI KICHAPO 4-3 KUTOKA KWA WAHASIMU WAO DMV

Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Modest J. Mero akiwapongeza timu ya DMV na kuwashukuru kwa kuweza tenga muda wao na kuja kushiriki katika mechi ya kirafiki kati yao na wenyeji New York iliyochezwa siku ya Jumamosi July 15, 2017 Lincoln Park Jersey City, New Jersey na DMV kufanikiwa kuibanjua timu ya New York kwa bao 4-3. Pamoja na refa kuonekana kuibebea mbeleko timu ya New York vijana wa DMV walikua imara na kuweza kuibuka kidedea katika mechi hIyo ambayo timu ya New York walikua wakitaka kuitumia kama mechi ya kulipiza kisasi baada ya timu hiyo inayotoka katika jiji lisilolala kufungwa goli 5-0 kwenye sikukuu ya Memorial day mechi iliyopigwa Jumamosi Mei 24, 2014 katika uwanja wa Walker Mills Park uliopo Walker Mills Rd, Capitol Heights,Maryland.
 Kocha mchezaji na timu kepten wa timu ya DMV Liberatus Mwang'ombe akitoa shukurani zake kwa Mhe. Balozi na Jumuiya ya New York kwa kuendeleza ijirani mwema kwa kuwakaribisha kuja kucheza mechi na wao
 Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Modest J. Mero akimkabidhi kocha mchezaji na timu kepteni wa timu ya DMV Liberatus Mwang'ombe kombe la mbuzi ambalo baada ya kukabidhiwa Libe aliirudisha kwa wenyeji ili uchomwe nyama nawaweze kuila pamoja na wenyeji wao.
Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania kwenye Umoja wa Mataifa, Mhe. Modest J. Mero wanne toka kushoto akiwa na wageni wake akiwemo Jaji Mkuu mstaafu Mhe. Jaji Othman Chande (mwenye fulana ya buluu) wakifuatilia mechi kali kati ya timu ya DMV na timu ya New York.
Kwa picha zaidi bofya soma zaidi


No comments: