Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni(wa pili kulia), Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala(wa kwanza kulia) na Mkuu wa Chuo cha Uhamiaji – TRITA, Kamishna wa Uhamiaji Maurice Kitinusa(wa kwanza kushoto) wakipokea vifaa vya TEHAMA toka kwa Balozi wa China Nchini Tanzania Dr.Lu Youqing(wa pili toka kushoto). Makabidhiano ya vifaa hivyo yamefanyika Julai 12, 2017 katika Chuo cha Uhamiaji – TRITA Mkoani Kilimanjaro.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala(kulia) na Balozi wa China nchini Tanzania Dr.Lu Youqing(kushoto) kwa pamoja wakisaini hati za makabidhiano ya vifaa vya TEHEMA vilivyotolewa na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China. Wengine wakishuhudia tukio hilo ni Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni(wa pili kulia), Kamishna wa Uhamiaji Maurice Kitinusa(wa pili toka kushoto) na Maafisa toka Ubalozi wa China.
Mkuu wa Kitengo cha TEHAMA katika Chuo cha Uhamiaji – TRITA, Mkaguzi wa Uhamiaji Zawad Chazuka akitoa maelezo ya kitaalam kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni namna vifaa hivyo vitakavyoleta ufanisi wa kazi chuoni hapo.
Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala(kushoto) akifafanua jambo kwa Balozi wa China Nchini Tanzania Dr.Lu Youqing walipotembelea Maktaba ya Chuo hicho.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Mhe. Mhandisi Hamad Masauni akiagana na Kamishna Jenerali wa Uhamiaji, Dkt. Anna Makakala mara baada ya hafla fupi ya makabidhiano ya vifaa vya TEHAMA kutoka ubalozi wa China(Picha zote na Leslie Mbota, PRO -TRITA).
No comments:
Post a Comment