Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Dully Sykes, akiwasikilizisha nyimbo zake mashabiki waliofurika katika Ukumbi wa Dar Live usiku wa kuamikia leo katika shoo ya kuwapa heshima waanzilishi wa Muziki wa Bongo Flava nchini ambapo 'mizinga' mitano ya kuheshimu kazi yao hiyo ilipigwa.[/caption]
Usiku wa kuamkia leo Jumapili ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani wa Dar Live uliopo Mbagala Zakhem jijini Dar kulikuwa na shoo ya heshima kwa Bongo Flava waanzilishi wa muziki huo waliowahi kutamba enzi hizo walipigiwa mizinga mitano kabla kuanza mambo.
Shoo hiyo iliyoandaliwa na kituo cha Redio na Runinga cha East Africa Television na Radio ya East Afrika kupitia kipindi chake cha Planet Bongo baada ya kupigwa mizinga hiyo umati uliofurika ukumbini hapo ulitulia dakika moja kuwakumbuka waanzilishi wa muziki huo waliotangulia mbele za haki.
Baadhi ya wasanii waliotajwa majina yao wakiwa mbele za haki ni pamoja na Albert Mangwair, Mr Ebbo, Dogo Mfaume, Langa Kileo, Complex na Vivian ambao wote nyimbo zao zilizowahi kutikisa zilipigwa. ...Akiendelea kuwapagawisha mashabiki.[/caption]
Tukio la kuwakumbuka waasisi hao lilipopita wasanii na makundi mbalimbali yaliyowahi kutikisa enzi hizo yalianza kuvamia jukwaa moja baada ya jingine na kupiga nyimbo zao zilizowahi kutamba.
Mashabiki wa burudani walionekana kukunwa sana na burudani hiyo ambapo baadhi walisikika wakisema hiyo ndiyo ilikuwa Bongo Flava ya ukweli.
Katika burudani hiyo alianza kuvamia jukwaa Z Anto, University Corner, LWP, Daz Nundaz Family chini ya Daz Baba, Wagosi wa Kaya, Solid Ground Family, Dully Sykes, Mandojo na Domokaya, Tid, Jaymoe, Dudu Baya, Manduli Boy, Mabaga Fresh, Afande Sele, Ispector Haruni ambapo mkali wa Temeke, Juma Nature ndiye aliyefunga kazi.
[caption id="attachment_151489" align="aligncenter" width="800"] Mashabiki wakimshangilia Dully Sykes.[/caption]
Katika burudani hiyo kila msanii aliyepanda jukwaani alitaka kujidhihirisha kama bado yuko vizuri kwenye gemu maana makamuziki hayakuwa ya chini, ambapo Kundi la Mabaga Fresh lilionekana kuupagawisha ukumbi huo hasa waliposhusha kibao chao kilichowawahi kutamba cha Tunataabika.
Kibao hicho kiliufanya ukumbi huo ulipuke kwa mayowe ya kushangilia huku DJ Snox naye akiwachagiza kwa swaga za kiulemavu huku akiinadi tafsiri ya Mabaga Fresh kuwa Ulemavu fresh tu.
[caption id="attachment_151493" align="aligncenter" width="800"] Msanii mkongwe Khalid Mohammed aka TID Mnyama akifanya makamuzi. ...TID akiendelea kufanya makamuzi
Msanii mkongwe mwengine, Dudu Baya, akiongea na mashabiki wakati wa shoo hiyo. ...Akipiga shoo. Kundi la Mabaga Freshi wakikumbushia enzi zao. ...Makamuzi yakiendelea Msanii mkonge, Afande Sele, akiwapagawisha mashabiki wa Bongo Fleva. Inspekta Haroun akikumbushia enzi zake kwa mashabiki. Juma Nature (kushoto) na Dollo wakifanya makamuzi. Inspekta (kushoto) akiimba na Juma Nature. Jay Moe akiwapa burudani mashabiki. Wagosi wa Kaya wakiwapa burudani mashabiki kwa nyimbo za tangu enzi zao mpaka sasa.[/caption]
(Picha/Habari na Richard Bukos/GPL)
No comments:
Post a Comment