Advertisements

Wednesday, July 19, 2017

WAZIRI MKUU MH MAJALIWA ASHIRIKI MAZISHI YA LINAH MWAKYEMBE

  
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akitia saini kitabu cha maombolezo baada ya kuwasili nyumbani kwa Waziri wa Habari, Utamaduni,Sanaa na Michezo, Dkt. Harrison Mwakyembe  kushiriki katika mazishi ya mke wa Waziri huyo, Linah George Mwakyembe yaliyofanyika Kyela Julai 19, 2017.  Kulia ni  mkewe Mary(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

 
 Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa na mkewe Mary  (wapili kushoto) wakishiriki katika ibada ya mazishi ya Marehemu, Linah George Mwakyembe, Mke wa Waziri wa Habari,Utamaduni, Sanaa na Michezo,  Dkt Harrison Mwakyembe katika mazishi yaliyofanyika  Kyela Julai 19, 2017.  Wengine pichani kutoka kushoto ni Waziri Mkuu Mstaafu, John Malecela, Mkuu wa Mkoa wa Mbeya  Amos Makalla, Spika wa Bunge, Job Ndugai, Naibu Spika wa Bunge, Dkt. Tulia Ackson Mwansasu kulia ni Waziri wa  Kilimo na Mifugo,   Dkt . Charles Tizeba. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

 

No comments: