Advertisements

Monday, July 17, 2017

WAZIRI PROFESA NDALICHAKO AFANYA ZIARA MKOANI IRINGA

Mheshimiwa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na Mbunge wa Iringa mjini Mh. Mchungaji Peter Msigwa katika Shule ya Viziwi, kulia ni Mbunge Viti Maalum Mhe Zainab Mwamwindi akisikiliza na katikati ni Mbunge wa viti Maalum Iringa Mh. Ritha Kabati.

Mheshimiwa Profesa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi alifanya ziara ya ghafla katika shule Mkoani Iringa. Alitembelea shule zinazofundisha watoto wenye mahitaji maalum za Makala Wilaya ya Mfundi, Shule ya viziwi Mtwivila, Shule ya sekondari ya wasichana Mtwivila na shule ya sekondari ya Lugalo. Nia ya ziara ni pamoja na kukagua vifaa vya kufndishia ambvyo serikali imetoa. Pia alipta fursa ya kusalimia wanafunzi na walimu. Katika ziara hiyo aliongzana na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe Amina Masenza, Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Bi wamoja Ayoub, Wakuu wa wilaya ya Mufindi Mheshimiwa Jamhuri David na Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela. Pia wabunge waheshimiwa, Ritta Kabati, Zainab Mwamwindi na Mch Peter Msigwa
Mheshimiwa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Richard Kasesela kushoto ni Mbunge wa jimbo la Iringa mjini Mchungaji Peter Msigwa.
Mheshimiwa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza pamoja na viongozi mbalimbali mkoani Iringa wakifurahia jambo na wanafunzi wa shule ya maalum ya viziwi mkoani humu
Mheshimiwa Joyce Ndalichako Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi akizungumza na Mh. Ritha Kabati akiwa katika picha ya pamoja na wanafunzi
Profesa Ndalichako nawanafunzi wa Iringa Girls 
Profesa Ndalichako akiongea na wananfunzi wa Shule ya sekondari Lugalo kidato cha 5

No comments: