ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, August 12, 2017

DELINA GROUP YADHAMINI JEZI MTANANGE WA SIMBA NA YANGA COLUMBUS, OHIO LABOR DAY



Mkurugenzi wa Delina Group Bw. Davis Mosha ametoa jezi za Simba na Yanga pamoja na kombe kwenye mtanange wa Simba na Yanga utakaochezewa Columbus, Ohio Jumamosi ya Sept 2, 2017 katika uwanja wa Avery Park wenye anuani 7501 Avery Rd, Dublin, OH 43017. Mtanage huo utakao washirkisha wachezaji Nico Njohole anayekuja toka Uingereza akiambatana na mdogo wake Renatus Njohole anayechezea Norway ambao wote kwa pamoja nyakati tofauti waliowahi chezea Simba ya jijini Dar, mchezaji mwingine atayecheza mtanange huo ni Deo Ngassa aliyewahicheza Yanga na Kipa Pual Rwechungura aliyewahichezea Pamba ya Mwanza.

Wachezaji wengine wanaotoka Ulaya kucheza mtanange wa Simba na Yanga ni Jameel Silia na Abui Hamisi waliowahichezea Moro United ambao kwa sasa wanachezeatimu yao yaKilimanjaro nchini Sweden ambao wote kwa pamoja wataungana na Jack Pemba ambaye yeye atachezea Simba na baadae atakabidhi kombe kwa mshindi wa mechi hiyo inayosubiliwa kwa hamu na mashabiki wa mpira wa miguu mjini Columbus na majimbo mengine watakao kuja Ohio kusherehekea Labor Day itakayopamba moto kuanzia Sep 1-3.


Kabla ya mechi hiyo itafanyika Bonza ya mpira wa kikapu itakayowashirikisha wachezaji waliowahichezea timu za Pazi,Vijana, Don Bosco na kwengine Tanzania. Bonaza hilo litafanyika katika uwanja wa ndani ulipo mji wa Dublin wenye anuani ya 6615 Dublin Center Dr, Dublin, Oh 43017.

Bonanza la mpira wa kikapu na mtanage wa Yanga na Simba ni sehemu ya shamrashamra ya sherehe ya Labor Day hiyo itakayofanyika Columbus, Ohio na kuwashirikisha Watanzaniawa jimbo hilo kujumuika pamoja marafiki zao wengi watakao kuja Columbus kutoka Canada na sehemu nyingine Ulaya.

Sherehe hii itapambwa na mwanamitindo nguli Asya Idarous Khamsini na Missy Temeke watakaofanya onyesho la mavazi usiku wa Ijumaa Sep 1, katika ukumbi wa 4257 Eastland Square Dr, Columbus, OH 43243 chini ya Dj Burundi na usiku huo utakua usiku wa Afrika,

Usiku wa Jumamosi Sep 2 utakua ni usiku wa vijana wa zamani kukumbuka enzi zao Watanzania kutoka kila pembe ya Dunia wanatarajiwa kuhudhuria mnuso huo mkongwe kupita yote uliobeba jina la OLD SCHOOL REUNION Labor of Love. Mji wa Columbus una historia ndefu ya minuso ya kuwakutanisha Watanzania wengi zaidi kuliko sehemu nyingine yeyote kwa kutokana na kuwa katikati ya Marekani. Usiku huo utakaokua chini ya madj bora Amerika ya kaskazini Dj Dennis (Funky House)na Dj Luke Joe(the mixmaster).

Siku ya Jumapili kutakua na nyama choma Avery Park wenye anuani 7501 Avery Rd, Dublin, OH 43017 na baadae usiku itafuatiwa na usiku wa Reggae na hiyo itakua imekamilisha siku tatu za kula bata mpaka kuku aone wivu. Karibu sana Columbus, Ohio The Haert of Tanzanian's Entertaiment in the USA.

No comments: