ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 21, 2017

Ester Bulaya Augua Ghafla Akiwa Rumande

Mbunge  wa Bunda Mjini, Ester Amos Bulaya (Chadema) amelazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Tarime mkoani Mara usiku wa kuamkia leo baada ya kuugua ghafla akiwa rumande ambako alikuwa ameshikiliwa na Jeshi la Polisi Kanda ya Tarime Rorya baada ya kumkamata akiwa hotelini kwa madai ya kutaka kufanya mkusanyiko usio halali.

Taarifa za kulazwa kwa Bulaya zimethibitishwa na  Mbunge wa viti maalumu mkoa wa Mara Joyce Sokombi (CHADEMA) ambapo amezungumzia hali ya Mbunge huyo kwa sasa, na kusema kwamba hali yake bado haijatengemaa kwani amepewa rufaa kwenda hospitali ya mkoa.


Mh. Sokombi amesema presha ya Ester Bulaya  bado ipo chini, kiasi kwamba wameshindwa kumsafirisha kwenda hospitali kubwa, hivyo wanasubiri madaktari wamsaidie kurudisha hali ya presha yake, ndipo wamtoe hospitali.

Pia Mh. Sokombi amesema kwa sasa Bulaya ameshapatiwa dhamana akiwa hapo hospitalini

No comments: