Familia ya Marehemu Mother Jessie Amour ya Kilimani Zanzibar, inatangaza kuwa mazishi ya Marehemu Wilson Charles Amour yatafanyika kesho Jumapili Aug 27, 2017.
Shughuli za mazishi zitaanza saa tano kamili asubuhi nyumbani Kilimani.
Ibada ya mazishi itafanyika katika Kanisa Kuu la Kristo Mkunazini kuanzia saa nane mchana, na baadaye itafuatiwa na ibada ya kuupumzisha mwili wa Marehemu Wilson itakayofanyika katika makaburi ya Mwanakwerekwe Zanzibar. Ahsanteni
1 comment:
poleni sana sana kabisa wafiwa wote ndugu,jamaa na marafiki.mwenyezi mungu akupeni moyo wa kustahamil katika kipindi hichi cha msiba.poleni sana.Na mwenyezi mungu amlaze mahali pema peponi uncle Charles amour.
Post a Comment