Advertisements

Tuesday, August 22, 2017

"Nimefunga mjadala wa Rambirambi" RC Gambo


RC Gambo akiwakabidhi wazazi wa Doreen Mshana jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi.
RC Gambo akiwakabidhi wazazi wa Wilson Tarimo jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi.

RC Gambo akimkabidhi mzazi wa Shadhia jumla ya Shilingi Milioni 7.75 ikiwa ni bakaa ya michango ya rambirambi
Kushoto ni mtoto Shadhia na Kulia ni mtoto Wilson wakitoka nje ya jengo la ofisi ya Mkuu wa mkoa
Mhe Gambo akisalimiana na mtoto Doreen Mshana
Mhe Gambo katika picha ya pamoja na manusura wa ajali ya Lucky Vincent walipotembelea ofisi yake mapema hii leo.

Hatimaye utata uliokuwa umeenea wa kuwepo kwa ufujaji na matumizi mabaya ya fedha kiasi cha milioni 285.49 zilizokuwa zimechangwa na wadau pamoja na serikali kwa ajili ya rambi rambi ya vifo vya ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent umekwisha baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha Mrisho Gambo kukabidhi milioni 23.27 kwa wazazi wa watoto walionusurika katika ajali hiyo
Akikabidhi fedha hizo mbele ya waandishi wa habari ambapo kila mzazi amepata Milioni 7.75, Bw. Gambo amesema fedha hizo zilikuwa zimebaki baada ya matumizi ya shughuli za mazishi kwa watoto 32 walimu wawili na dereva waliokuwa wamekufa katika ajali hiyo na matumizi mengine yakiwemo ya wazazi waliokuwa nchini marekani kwa ajili ya kuwauguza watoto wao na kwamba matumizi ya fedha hizo watapanga wao wenyewe.
Katika hatua nyingine Bw Gambo alisema Serikali imekubali kutoa wataam wa saikolojia kwa ajili ya kuendelea kuwasaidia watoto walionusurika katika ajali ya basi la wanafunzi ili kuwaweka sawa na pia kuwaandaa kufanya mtihani wa darasa la saba unaowakabili mnamo mwezi Septemba.
Aidha Bw, Gambo amesema kazi ya kutoa tiba ya kisaikolojia pia ilishafanyika kwa wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent .
Wakizungumza baada ya kukabidhiwa Fedha hizo wazazi wa watoto hao wameishukuru serikali na wafadhili kutoka marekani kwa msaada mkubwa kwa watoto wao tangu mwanzo hadi sasa
Aidha wazazi hao wamesema pamoja na watoto wao kuwa nje ya shule kwa zaidi ya miezi mitatu wako tayari kufanya mtihani na kumaliza ELIMU ya msingi unaotarajiwa kufanyika mwezi September.
Kwa mujibu wa Bw Gambo baada ya kutokea kwa AJALI hiyo MWEZI May 2017 wadau MBALIMBALI na serikali walijitolea na kuchanga fedha na kupatikana zaidi ya milioni 285.49 ambazo nbaada ya matumizi zilibaki milioni 23.27 ambazo zimekabidhiwa leo.
Na kuhusu ombi la wazazi la kutaka watoto wao wafanye mtihani wa kumaliza elimu ya msingi licha ya kuwa nje ya shule kwa miezi zaidi ya mitatu Bw Gambo alisema kama wazazi wako tayari na wanaona watoto wao wana uwezo wa kufanya mtihani hakuna kipingamizi.
“Suala hili linawezekana ikiwa wazazi na watoto wataonyesha utayari wa kufanya mtihani huo,na hata mapema leo waziri wa elimu Mhe. Ndalichako ameshalizungumzia” alisema Gambo.
Kuhusu maelezo yalikuwa yameenea katika mitandao ya kijamii kuwa Bw Gambo ametakiwa kukabidhi fedha hizo kwenye mfuko wa kuendeleza watoto hao ulioanzishwa na shirika la Stemm huku wengine wakidai kuwa zipelekwe kuboresha Hosipitali ya Mkoa wa Arusha ya Mount meru Gambo alisema suala la kuanzisha mfuko na kuboresha hosipitali lina taratibu zake na sio lazima lisubiri fedha za chenji ya rambirambi
“Kama kuna mfuko wa ELIMU ni jambo jema na unaweza kuanzishwa na kuendelea ila hizo zilizopo wanakabidhiwa wazazi bila masharti yeyote.” alisisitiza Mhe Gambo.
Kuhusu madai kuwa serikali iliahidi kugharamia mazishi na baadaye yakagharamiwa na fedha za wadau Bw Gambo alisema fedha zilizotolewa na taasisi za serikali ni sawa na serikali imetoa na kwamba hayo ni masuala ya kisisasa ambayo asingependa yaingizwe kwenye masuala ya msingi yanayohusiana na maisha ya watu.
“Fedha zilizotolewa na taasisi mbalimbali za serikali mfano NSSF huwezi sema sio za serikali, nadhani ifike mahali tuache siasa nyepesi” alisema Mhe Gambo.
Alliongeza kuwa serikali imeshatenga Bilion 1.9 kwa ajili ya Hosipitali ya mkoa wa Arusha ya Mount Meru na kamwe serikali haiwezi kutumia michango hiyo kwa suala kama hilo na kuziita taarifa zilizosambaa mitandaoni kua ni za kizushi zenye nia ya kuichafua serikali.

No comments: