ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, August 23, 2017

PANYA WAMUONDOA RAIS BUHARI IKULU

Rais Muhammadu Buhari atatekeleza majukumu yake ya urais, kwa miezi mitatu kutoka nyumbani baada ya ofisi yake ya Ikulu kuharibiwa na panya na hivyo inabidi ifanyiwe matengenezo.
Miongoni mwa vifaa vilivyoharibiwa ni samani na viyoyozi. Uharibifu huo ulifanywa na panya wakati Buhari alipokuwa London, Uingereza kwa siku 103 akipatiwa matibabu ya maradhi ambayo hayajawekwa wazi.
"Kutokana na ofisi yake kubaki miezi mitatu bila kutumika, panya waliharibu samani na seti ya viyoyozi,” alisema Msemaji wa Serikali ya Nigeria, Garba Shehu na kusisitiza kwamba rais ana ofisi “iliyosheheni vifaa” nyumbani kwake na kwamba ataitumia “kikamilifu” kutekeleza majukumu yake.
Rais Buhari alirejea nchini Nigeria Jumamosi iliyopita na Jumatatu alizungumza na wananchi kupitia televisheni lakini hakugusia maradhi yanayomsumbua.

No comments: