Advertisements

Wednesday, August 9, 2017

RAIS DK. SHEIN AZUNGUMZA NA BODI YA WAKURUGENZI YA ZBC,UONGOZI WA WIZARA YA HABARI,UTALII NA MICHEZO

 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Habari, Utalii, Utamaduni na Michezo , Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya ZBC pamoja na Uongozi wa ZBC leo   katika kikao cha siku moja kilichofanyika katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya ZBC Bi. Nasra Mohamed (kulia)  alipokuwa akitoa taarifa ya Bodi yake  wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja, ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya  Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo na Uongozi wa ZBC, chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani),(kushoto) Mjumbe wa Bodi Nd,Ali Bakari.
 Mkurugenzi Mkuu wa ZBC Nd,Iman Othman Duwe (kulia) alipokuwa akitoa maelezo mbele ya Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani)  katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja leo  katika kikao cha siku moja cha  Uongozi wa Wizara ya Habari,Utalii,Utamaduni na Michezo, Bodi ya Wakurugenzi ya ZBC na Uongozi wa ZBC,ambacho kikao hicho kimejadili mambo mbali mbali ya kiutendaji ya ZBC na Bodi kwa pamoja, (kushoto) Mwenyekiti wa Tume ya Utumishi Serikalini Mhe.Mohamed Fakih.
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (katikati) alipokuwa akizungumza na Uongozi wa Wizara ya Biashara,Viwanda na Masoko,Bodi ya  Wakurugenzi  ya ZBS pamoja na Uongozi wa ZBS     katika kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika  Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja.
 Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya ZBS Prof Ali Seif Mshimba (kushoto)  alipokuwa akitoa taarifa ya Bodi yake  wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya  Biashara,Viwanda na Masoko na Uongozi wa  ZBS, chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), (kulia) Mwanasheria Mkuu wa Zanzibar Nd,Said Hassan Said
Mwenyekiti wa Bodi ya  Wakurugenzi ya ZBS Prof. Ali Seif Mshimba (kulia)  alipokuwa akitoa taarifa ya Bodi yake  wakati wa kikao cha siku moja kilichofanyika leo katika Ukumbi wa Ikulu Mjini Unguja,ambacho kilijumuisha Uongozi wa Wizara ya  Biashara,Viwanda na Masoko na Uongozi wa  ZBS, chini ya Mwenyekiti wa kikao hicho Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein (hayupo pichani), wengine ni baadhi ya Wajumbe wa Bodi ya ZBS wakisikiliza kwa makini taarifa hiyo (Picha na Ikulu).

No comments: