Serikali imetaifisha na kuamuru kuteketeza zaidi ya tani kumi na tano ya shehena ya vuiatilifu vya kilimo vilivyokamatwa na TPRI kwa kushirikiana na jeshi la Polisi mkoa wa Mtwara ambazo ziligundulika kutokuwa na sifa ya kutumika nchini ikiwemo kuisha muda wa matumizi na kutokuwa na usajili zilizotaka kusambazwa kwa wakulima wa Korosho huku mmiliki wake kampuni ya Hangzhou akitozwa faini ya zaidi ya shilingi milioni aribaini.
Wakili wa serikali mwandamizi mfawidhi mkoa wa Mtwara Ladislaus Komanya amesema hatua hiyo imefikiwa baada ya kukamtwa kwa shehena hiyo ambayo wamiliki wake kampuni ya walikuwa wanalengo la kusambaza dawa hizo kwa wakulima huku wakibadilisha nembo kuonesha kuwa zipo vizuri wakati zimeisha muda wa matumizi zingine hazikusajiliwa nchini na makosa mengine.
Kaimu mkurugenzi mkuu wa TPRI Dkt. Magreth Moleli amesema TPRI inamajukumu ya kulinda wakulima dhidi ya matendo yanayoathiri mazao ya kilimo na afya za bindamu hiyo sehena hiyo itateketezwa haraka iwezekanavyo.
Msajili wa viuatilifu Habibu Mkalana anasema adhabu hiyo itakuwa fundisho kwa wafanyabiashara wasiyo wadilifu na mkaguzi Mwandamizi kutoka TPRI Michael Sanga anasema operesheni hiyo itakuwa endelevu nchi nzima.
No comments:
Post a Comment