ANGALIA LIVE NEWS

Tuesday, August 22, 2017

TAASISI YA THPS YAZINDUA MPANGO MKAKATI WA KUSAIDIA MIFUMO YA AFYA 2016-2020

Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizungumza wakati wa Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020 na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS).  Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam. PICHA ZOTE NA MMG/KAJUNASON.
Wageni na wafanyakazi wa taasisi ya THPS waliohudhuria katika Uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020 na Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS). Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) Dkt. Augustine Massawe akizungumza katika uzinduzi wa Mpango Mkakati wa kusaidia mifumo ya afya wa miaka mitano ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016- 2020. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS), Dkt. Redempta Mbatia akizungumza juu ya uzinduzi wa Mpango Mkakati ya kusaidia mifumo ya afya na kuelezea malengo ya taasisi hiyo kwa miaka ijayo kati ya mwaka 2016-2020. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam. Mmoja ya vijana waelimisha Rika kutoka Zanzibara akitoa somo jinsi ya kujitambua.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya akizindua Mpango Mkakati wa kwanza wa kusaidia mifumo ya afya wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Redempta Mbatia na wadau wengine. Tukio hilo lilifanyika jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Wizara ya Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto (Afya), Dkt. Mpoki Ulisubisya (wa nne toka Kushoto) na Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi hiyo Dkt. Redempta Mbatia (wa tako kutoka kushoto) pamoja na wadau wa afya wakionyesha chapisho la Mpango Mkakati wa kwanza wa kusaidia mifumo ya afya  wa Taasisi ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016-2020.
---
Taasisi isiyo ya kiserikali ya Tanzania Health Promotion Support (THPS) inayosaidia Wizara za afya Tanzania Bara na Zanzibar kutoa kinga ya Virusi vya Ukimwi (VVU), huduma, matibabu na msaada kwa kuimarisha mifumo ya afya imezindua mpango mkakati wa kwanza wa miaka mitano.
Akizungumza katika uzinduzi huo wa mpango mkakati uliofanyika Jijini Dar es salaam leo.
Mwanzilishi na Mwenyekiti wa Bodi wa THPS, Dkt. Augustine Massawe alisema mpango mkakati wa kwanza wa taasisi hiyo ambao utatekelezwa kati ya mwaka 2016 mpaka 2020 umelenga kusaidia juhudi za Wizara ya afya, Serikali za mitaa, Washiriki wengine na Wadau kuhakikisha huduma bora za afya zinazoshugulikia afya ya umma ikiwemo magonjwa yanayoambukizwa na yasiyoambukizwa ili kuboresha matokeo ya afya kiujumla katika jamii.

 Dkt. Massawe alisema anatarajia mpango mkakati utazingatia mawazo kati ya wadau muhimu wa THPS na kujenga uamuzi wa pamoja wenye matokeo mazuri. “tunataka kugusa maisha ya Watanzania wengi kwa kuathiri ubora wa huduma za afya na kujenga taifa huru la VVU/UKIMWI. Nina matumaini kuwa mpango mkakati uliofikiriwa utakuwa kama chombo cha usimamizi wa taasisi katika kuweka vipaumbele, kuzingatia nishati na rasilimali, kuimarisha shughuli mbalimbali na kuhakikisha wafanyakazi na wadau wengine wanafanya kazi kwa malengo.

Akizungumzia juu ya uzinduzi wa mpango mkakati, Mkurugenzi Mtendaji wa THPS, Dkt. Redempta Mbatia alielezea malengo ya taasisi kwa miaka ijayo ni kutazamia mbali VVU/ UKIMWI na kushughulika na magonjwa mengine yenye vitisho katika jamii, kulenga katika uhamasishaji wa rasilimali na kuchunguza ushirikiano wa pamoja na sekta binafsi ili kuendelea kutoa huduma zake.

 “Mpango mkakati huu umekuja wakati muafaka ili kuhakikisha tunafikia idadi kubwa ya watu wenye mahitaji, wakati huo huo tukikuza na kuendeleza taasisi. Tunataka kuendelea kuzingatia maeneo muhimu ikiwa ni pamoja na huduma bora za afya, uwezo endelevu wa kifedha, utawala bora na uwajibikaji wa pamoja na wafanyakazi wenye uwezo na kujitolea.

 Kama taasisi mpya nchini Tanzania tunathamini sana Imani, msaada na fursa ya kutumikia watanzania inayotolewa na serikali kuu, serikali za mtaa, wafadhili, washirika watekejezaji na wadau wengine muhimu kutoka pande zote mbili za jamhuri. Mwisho kabla ya kumaliza tunashukuru kwa msaada endelevu wa kifedha na kiufundi kutoka kwa wafadhili wetu: Watu wa Marekani kupitia PEPFAR/ CDC na taasisi ya taifa ya afya Marekani (NHI) , UNAIDS , Chuo kikuu cha Harvard, Chuo kikuu cha Colombia na taasisi ya mfuko wa uwekezaji kwa watoto uliopo Uingereza”. 

Aidha Dkt. Mbatia alisisitiza kuwa mwelekeo wa mpango mkakati kwa miaka mitano ni kufaidika kwa njia ya moja kwa moja na isiyo ya moja kwa moja kwa mamilioni ya Watanzania. Mpango huo umesimama kama nguzo ya kuongeza na kubuni ufumbuzi wa afya bora ya kupambana na VVU na UKIMWI, mifumo ya utoaji afya na changamoto nyingine za afya zinazoathiri Watanzania.

1 comment:

Anonymous said...

Safi sana. Tunahitaji Taasisi nyingi kama hii, zenye malengo ya kuwaletea Watanzania maisha bora. MAREKEBISHO: NIH (National Institute of Health) na siyo NHI. Vile vile, Chuo Kikuu cha Columbia na siyo Colombia.