ANGALIA LIVE NEWS

Monday, August 7, 2017

TADB YATOA ‘SAPOTI’ NANE NANE KITAIFA

Meneja wa Mikopo wa TADB, Samuel Mshote (kulia) akiwaonesha wanahabari ujumbe wa Maadhimisho ya Nane Nane kwa mwaka 2017 kabla ya makabidhiano rasmi ya fulana na kofia kwa Kamati ya Maandalizi ya Nane Nane kitaifa mjini Lindi.
Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (wapili kushoto) pamoja na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kulia) wakisoma ujumbe wa maadhimisho ya Nane Nane kwa mwaka 2017. Wanaoshuhudia ni Mkuu wa Wilaya ya Lindi, Bw. Shaibu Ndemanga (kushoto) na Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Simon Migangala (kulia).
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akimkabidhi fulana na kofia Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (kushoto) zitakazotumika wakati wa kilele wa Maadhimisho ya Siku na Nane Nane kitaifa mjini Lindi.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB), Bw. Francis Assenga (wapili kulia) akimkabidhi fulana na kofia Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Godfrey Zambi (kushoto) zitakazotumika wakati wa kilele wa Maadhimisho ya Siku na Nane Nane kitaifa mjini Lindi.

Na Mwandishi wetu,

Katika kudhirisha umuhimu wa Siku ya Nane Nane Benki ya Maendeleo ya Kilimo Tanzania (TADB) imeunga mkono kwa kutoa fulana na kofia zitakazovaliwa katika siku ya kilele cha maadhimisho hayo.

Akizungumza wakati wa makabidhiano ya vifaa hivyo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Wageni Maalumu uliopo katika Viwanja vya Ngongo mjini Lindi, Mkuu wa Mkoa wa Lindi, Bw. Godfrey Zambi alisema kuwa TADB imeonesha mfano kwa taasisi nyingine nchi kwa kutambua umuhimu wa Nane Nane inayofanyika kitaifa mkoani humo.

“Tunaishukuru sana TADB kwa mchango huu ambao kwa hakika utang’arisha maadhimisho yetu,” alisema.

Bw. Zambi aliongeza kuwa mchango huo unachagiza kauli mbiu ya Maonesho hayo isemayo “Zalisha kwa tija mazao ya kilimo, mifugo na uvuvi ili kufikia uchumi wa kati”.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa TADB, Bw. Francis Assenga amesema kuwa Benki ya Kilimo imeunga mkono Maonesho hayo ya Nane Nane kwa kutambua umuhimu wa kilimo na kutimiza malengo ya Benki hiyo katika kusaidia kilimo nchini.

“Mchango huu unasadifu malengo ya kuanzishwa kwa TADB ambayo yanajumuisha Kusaidia upatikanaji wa utoshelezi na usalama wa chakula ambao ni endelevu nchini Tanzania; na Kuchagiza na kusaidia Mapinduzi ya Kilimo kutoka kilimo cha kujikimu kwenda cha kibiashara ili kuchangia kwenye ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini,” alisema Bw. Assenga.

Maadhimisho ya maenesho hayo yatafikia kilele siku ya tarehe 08 ambapo Mgeni rasmi wa anatarajiwa kuwa Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan.

No comments: