Advertisements

Thursday, August 17, 2017

Watumishi wa Umma Watakiwa Kubadilika

 Mganga Mkuu wa  Mkoa wa Kigoma Dkt. Paul Chote ambaye alikuwa mgeni rasmi wakati wa kufunga mafunzo kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa kuandaa bajeti, mipango na kutoa ripoti (PlanRep iliyoboreshwa) kutoka mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma akisisitiza  jambo kwa washiriki hao wakati akifunga mafunzo hayo.
 Muwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Elisa Rwamiago akizungumzia umuhimu wa mfumo huo katika kuleta mageuzi ya kiutendaji kwa washiriki wa mafunzo ya mfumo wa kuandaa bajeti, mipango na kutoa ripoti (PlanRep iliyoboreshwa) kutoka mikoa ya Katavi, Rukwa na Kigoma.
 Mkuu wa Timu ya mifumo ya TEHAMA kutoka PS3 bw. Desderi Wengaa akizungumza wakati wa hafla ya Kufunga mafunzo hayo.
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akizungumza muda mfupi kabla ya Hafla ya ufungaji mafunzo hayo iliyofanyika Mjini Kigoma. (Picha na Frank mvungi-Maelezo)

Frank Mvungi - Maelezo
Serikali imewataka watumishi wa umma katika mikoa na Halmashuri kubadilika na kutekeleza majukumu yao kwa kuzingatia mabadililko ya mifumo yanayofanywa kwa kushirikina na wadau wa maendeleo.
Akizungumza wakati akifunga mafunzo ya mfumo wa kielektroniki utakaotumika kuandaa mipango,bajeti na kutoa ripoti yaliyowashirikisha washiriki kutoka Mikoa ya Katavi, Rukwa na kigoma, Mganga mkuu wa mkoa wa Kigoma ambaye alikuwa mgeni rasmi katika hafla hiyo Dkt. Paul Chote amesema dhamira ya serika ni kuwawezesha watumishi wake kutekelza majukumu yao kwa ufanisi hasa katika kuwahudumia wananchi.
“Mfumo huu sio wa majaribio hivyo ni wajibu wa kila mshiriki kurudi katika mkoa na halmashuri na kuhakikisha kuwa anajenga uwezo kwa watumishi ambao hawakushiriki katika mafunzo haya kwa kuwa mfumo huu unahitaji uwajibikaji wa pamoja” alisisitiza Chote.
Akifafanua Dkt. Chote amesema kuwa washiriki wa mafunzo hayo wana jukumu kubwa lakutumia weledi na ujuzi waliopata kuleta mageuzi chanya katika maeneo yao ili azma ya serikali kutoa huduma bora itime. 
Kwa upande wake Muwakilishi kutoka Ofisi ya Rais TAMISEMI bw. Lisa Rwamiago amesema kuwa vituo zaidi ya elfu 22,000 vya kutolea huduma vitaunganishwa katika mfumo huo wa Kitaifa hali itakayofanya Tanzania kuwa nchi ya kwanza kusini mwa Afrika kwa kuwa na mifumo bora yakutolea huduma.
“Nashukuru PS3 kwa ushirikiano uliopo kati yake na TAMISEMI na umewezesha kutekelezwa kwa miradi yenye tija hasa kwa wananch”.Alisisitiza Rwamiago
Akifafanua Rwamigo amesema kuwa watumishi katika Mikoa na Halmashuri lazima waoneshe kwa vitendo namna tofauti ya kutekelza majukumu yao kwa kutumia mfumo huo wa kielektroniki ulioboreshwa ambao ni (web based).
Mradi wa PS3 unalenga kushirikiana na Serikali katika kuboresha matumizi ya rasilimali zilizopo ikiwemo fedha, rasilimali watu na mifumo katika ngazi ya kutolea huduma kama vile vituo vya Afya,Zahanati,Hosipitali na katika sekta ya elimu.
Kutokana na maboresho na kurahisishwa kwa Teknolojia,mfumo huu mpya wa PlanRep umefanywa kuwa ‘web based’ hivyo utawezesha Halmashuri kuingiza taarifa za Mipango na Bajeti moja kwa moja kwa njia ya mtandao na kuweza kutumwa kwenye mfumo mmoja uliopo Ofisi ya Rais TAMISEMI na hatimaye kuingizwa kwenye bajeti kuu ya mwaka husika.

No comments: