Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Sheikh Abdurahman Muhamed Ame (kushoto) akielezea juu ya Mkutano wa 48 wa Jumuiya hiyo mbele ya waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 September hadi 1 Oktoba leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya hiyo Tahir Mahmood Chandhry.
Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Tahir Mahmood Chandhry (katikati) akifafanua jambo juu ya Mkuatano Mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo mbele ya waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika tarehe 30 September hadi 1 Oktoba, leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya hiyo Sheikh Abdurahman Muhamed Ame, Kulia ni Katibu wa Uchapishaji wa Jumuiya hiyo, Jamil Mwanga.
Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Tahir Mahmood Chandhry (katikati) akisoma barua iliyotumwa na Khalifatul Masihi Mkuu wa Jumuiya hiyo duniani Mirza Mansoor Ahmad mbele ya waandishi wa habari kuelekea katika Mkutano Mkuu wa 48 utakaofanyika tarehe 30 September hadi 1 Oktoba mwaka huu, leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Sheikh Abdurahman Muhamed Ame. Kulia ni Kulia ni Katibu wa Uchapishaji wa Jumuiya hiyo Jamil Mwanga.
Na Neema Mathias na Thobias Robert-MAELEZO
Hayo yameelezwa jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya hiyo Sheikh Abdurahman Ame alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari ambapo alisema kauli mbiu ya mkutano huo ni, “Muislam wa kweli ni yule ambaye watu wengine wote wako salama dhidi ya shari ya ulimi wake na mikono yake.”
Kauli mbiu hiyo inawaasa waislam duniani kote kwamba, wana haja ya kuishi na kutenda kwa namna ambayo watu wengine watakuwa mashahidi kwamba Islam ni dini ya amani.
“Mkutano huo siyo wa kisiasa wala si mkutano dhidi ya madhehebu mengine duniani bali unawakumbusha waumini wa kiislamu juu ya masuala na wajibu wao wa kidini,” alifafanua Sheikh Ame.
Aidha, alisema kuwa jumuiya hiyo ndiyo pekee miongoni mwa jumuiya za kiislam iliyo na utaratibu wa ukhalifa ikiongozwa na kiongozi mmoja anayesimamia utendaji katika kila nchi duniani kote. Hapa nchini jumuiya hii ina upekee kwani ndiyo ya mwanzo kutafsiri Qurani tukufu kwa lugha ya Kiswahili mwaka 1953.
“Jumuiya hii imekuwa ikifanya mikutano yake mikuu kila mwaka kwa lengo la kukumbusha misingi sahihi ya dini tukufu ya Islam, kukuza udugu na urafiki miongoni mwa wana jumuiya na wananchi kwa ujumla na kuhamasisha uwepo wa amani katika jamii,” alieleza Sheikh Ame.
Akiwakilisha barua ya kiongozi mkuu wa jumuiya hiyo duniania aitwaye,Hadhrat Mirza Mansoor Ahmad, Amir na Mbashiri Mkuu wa jumuiya hiyo hapa nchini Tahir Chandhry, aliwasilisha alieleza kuwa washiriki hawana budi kuliombea taifa amani na kujizatiti katika kuienzi jumuiya kwa maendeleo ya dini ya uislam duniani kote.
“Ninawahimiza nyote mjizatiti kutimiza masharti ya baiat zenu hususan kuienzi taasisi ya kiroho ya Khilafat-e-Ahmadiyy. Jueni ya kwamba maendeleo ya Jamaat, kuenea kwa Islam na kupatikana kwa amani duniani, kimsingi vinaambatana na taasisi ya Ukhalifa,” alieza Chandhry.
Aidha aliongeza kuwa, ni wajibu kwa kila mwananchama wa jumuiya hiyo popote alipo duniani anapaswa kuonesha mapenzi, nguvu na wajibu wao katika kuchangia maendeleo ya taifa hili na kufanya kila kinachowezekana kudhibiti madaraka yao.
“Hivi ni kama vita kila mmoja anapaswa kuwa mzalendo katika nchi yake, kutii katiba na kufanya mambo ya maendeleo kwa ajili ya taifa letu, kwani bila amani hakuna haki,” alieleza Chandhry.
Jumuiya ya Ahmadiyya ilianzishwa na Hadhrat Mirza Ghulam Ahmad a.s wa Qadian India mwaka 1889, nchini Tanzania ilisajiliwa rasmi mwaka 1934 ambapo mbali na kutoa huduma za kiroho imekuwa mstari wa mbele kutoa huduma za kijamii pasipo kujali itikadi za wananchi.
Huduma ambazo zimekuwa zikitolewa na jumuiya hii ni kuchimba visima vya maji, huduma za afya pamoja na elimu ya sekondari katika Mkoa wa Dar es Salaa na elimu ya awali na msingi katika mkoa wa Morogoro pia jumuiya hiyo ipo katika hatua za mwisho za uanzishaji na ukamilishaji wa kituo cha radio nchini.
Jumuiya Ahmadiyya ni ya kimataifa iliyoenea katika nchi 210. Mkutano wa mwaka huu utahudhuriwa na washiriki kutoka nchi za nje za Kenya, Uganda, Burundi, Malawi, Msumbiji na Uingereza.
No comments:
Post a Comment