Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Mkoani Singida Mhandisi Jackson Masaka akimkaribisha Meneja Mawasiliano na Uhusiano Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi.Sylvia Lupembe Ofisini kwake wakati wa ziara ya Taasisi hiyo wilayani hapo kuangalia miradi wanayoifazili.
Wazazi wa Wanafunzi wa kabila la kihadzabe wanaojengewa bweni na bwalo na Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) katika shule ya msingi Munguli wakiwa katika eneo la Ujenzi wa Mradi huo
Moja ya Nyumba ambayo ipo katika mradi wa nyumba za Walimu ikiwa imekamilika katika Shule ya Msingi Isanzu Wilayani Mkalama kwa ufazili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA).
Mwenyekiti wa Kijiji cha Senene(Kulia) Bw.Athumani Jumanne na Mwalimu Mkuu wa Shule ya Msingi Kibololo Mwl.Alphone Michael wakiwa wamekalia moja ya madawati 130 yaliyotolewa kwa shule za msingi Senene na Kibololo Wilayani Mkalama,Singida ikiwa ni ufazili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania.
Kamati ya Ujenzi Shule ya Msingi Kibololo wakishiriki kuandaa eneo litakalojengwa vyoo na madarasa matatu kwa ufazili wa Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) Wilayani Mkalama,Singida.
Meneja Mawasiliano na Uhusiano Mamlaka ya Elimu Tanzania(TEA) Bi.Sylvia Lupembe akifurahia jambo na Wazazi wa wanafunzi wa Kabila la Kihadzabe mara baada ya kukagua miradi ya bwalo na bweni inayofaziliwa na Mamlaka hiyo Wilayani Mkalama,Mkoani Singida.
Na Daudi Manongi,MAELEZO
No comments:
Post a Comment