Advertisements

Thursday, September 21, 2017

MHE. DKT. AUGUSTINE MAHIGA, WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI AMWAKILISHA MHE. RAIS DKT. JOHN POMBE JOSEPH MAGUFULI KATIKA MKUTANO 72 WA UMOJA WA MATAIFA

Mhe. Dkt. Agustine Mahiga MP, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki ameongoza Ujumbe wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Mkutano wa 72 wa Umoja wa Mataifa (72nd session of the United Nations General Assembly) inayofanyika Septemba 12, 2017 hadi Septemba 25, 2017. Pamoja na Mhe. Waziri Dkt. Augustine Mahiga MP, wengine waliyopo kwenye Ujumbe uliyomwakilisha Mhe. Rais Dkt. Rais John Pombe Joseph Magufuli ni Mhe. Modest J. Mero, Mwakilishi wa Kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Ujumbe wa Kudumu wa Umoja wa Mataifa, New York (Permanent Mission of Tanzania to the United Nations), Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico na Balozi Celestine J. Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikianko Wa Kimataifa, Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.
Pichani mbele: Mhe. Dkt. Agustine Mahiga, MP, Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki; Mhe. Balozi Modest J. Mero, Mwakilishi wa kudumu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, New York; Mhe. Wilson M. Masilingi, Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Marekani na Mexico na nyuma ya Waziri, Balozi Celestine J. Mushy, Mkurugenzi wa Idara ya Ushirikianko Wa Kimataifa

Wajumbe (delegates) wawakilishi wa mataifa mbalimbali ya dunia wa Umoja wa Mataifa wakimsikiliza Mhe. Rais Donald J. Trump, Rais wa Marekani katika hotuba yake kwa Umoja Mataifa

1 comment:

Anonymous said...

Sijui kwanini baba Jessica hataki kuja kwa trump,au anaogopa ndege za masaa mengi nini?mhh