Waziri wa Utamaduni Sanaa na Michezo Harrison Mwakyembe amesema amepiga marufuku mashindano ya miss Tanzania na Tuzo za muziki
Amesema mashindano ya Miss Tanzania yamegubikwa na ubabaishaji kwenye utoaji wa tuzo na wamekuwa wakiwasotesha watoto wetu kwa mwaka mzima wakijiandaa na tuzo hizo lakini mwisho kuwapa zawadi inakuwa ni usumbufu
Ameongezea kwa watakaotaka kuandaa mashindano hayo zawadi wanazoahidi kuwapa washindi ziwekwe ofisini kwake
Kwa sasa wanakaa chini na wadau wa burudani juu ya mashindano hayo ila wanataka ziwe na (guaranteed sustainability) muendelezo wa uhakika na sio kufanyika kwa kubahatisha
Kwenye tuzo za muziki waziri amesema tuzo za muziki zilikuwa zikitegemea watu wakinuna basi hakuna tuzo hizo na pia zinahitaji marekebisho.
Chanzo: Times FM
No comments:
Post a Comment