Advertisements

Sunday, September 17, 2017

Tamasha linaitwa Dodoma Mpya Concert, nimeanza Tarehe 16/9/2017 Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.


Ndugu Josias Charles ambaye ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Millennium Stars Entertainment akitoa neno la Ukaribisho kwa wageni na wasanii waliojitokeza Katika Tamasha hili
Kwa kifupi Tamasha linaitwa Dodoma Mpya Concert, nimeanza Tarehe 16/9/2017 Wilaya ya Mpwapwa Mkoani Dodoma.


Tamasha hili limeandaliwa na Kampuni ya Millennium Stars Entertainment na lengo kubwa ni Kuhamasisha Sanaa kuwa chanzo kikuu cha Mapato Nchini na kuwa sehemu ya Ali Rasmi.


Kupitia Tamasha hili Vikundi 10 vya sanaa vitakavyoshiriki chini ya Baraza la Sanaa la Taifa BASATA.

Vikundi mbalimbali vya sana vikitumbuiza kwenye Tamasha la Dodoma Mpya Concert liliofanyika Wilayani Mpwapwa Jumamosi ya Tarehe 16/9/2017


Shughuri mbalimbali za Kiujasiliamali zinazofanywa na vikundi mbalimbali vya sanaa ikiwa ni pamoja na utengenezaji wa Vikapu maridadi vya Asili... Kujali hicho kinauzwa kwa Sh. 60,000 za kitanzania
Kwa taswira zaidi ya nini kilibamba kwenye Tamasha hili jitiririshe kwenye soma zaidi.

Afisa wa NHIF Bi. Mwanawewe akifuatiliakwa ukaribu Tamasha la Dodoma Mpya Concert.


Afisa Utamaduni wa Wilaya ya Mpwapwa Bi. Editha Robert akitoa nasaha kwa Vikundi vya sanaa Kutumia sanaa yao kama chanzo chao cha kipato.


Ma Afisa utamaduni wa Wilaya mbalimbali wa Kufuatilia Tamasha hili litakalofanyika kwa kila Wilaya

Mgeni Rasmi na muwakilishi wa Mkuu wa Wilaya ya Mpwapwa akifuatilia kwa ukaribu Vikundi mbalimbali vya sanaa vilivyoonyesha Umahili wa Hali ya Juu kabisa katika sanaa.

Afisa Mahusiano wa NHIF alishindwa kuketi kwenye Kiti na kulazimika kusimama mara kwa mara kupongeza kazi nzuri iliyokua ikifanywa na vikundi mbalimbali vya Sanaa.

Uongozi wa Baraza la Sanaa la Taifa ukiongozwa na Bwana Kurujira Maregesi ulivutiwa na tamasha lilivyoweza kufana. Tamasha hili liliambatana na Usajiri wa Vikundi vyote chini ya BASATA


No comments: