ANGALIA LIVE NEWS

Sunday, September 24, 2017

UJUMBE KUTOKA OFISI YA MAKAMU WA RAIS WAENDELEA NA ZIARA YA KUTEMBELEA MIGODI MKOANI TABORA.

Wachimbaji wadogo wa migodi wametakiwa kutunza mazingira katika maeneo yote yanayozunguka migodi pamoja na usalama kwa Wafanyakazi katika katika migodi hiyo. Rai hiyo imetolewa na ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais ulipotembelea mgodi wa Igulubi ulioko katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora katika ziara inayofanywa na Ujumbe huo wa kutembelea migodi ya Wachimbaji wadogo.

Wakiongea katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji na Mkurugenzi Msaidizi wa Mazingira Bi Magadalena Mtenga walisema kuwa utunzaji wa mazingira ni kitu cha muhimu sana na pia usalama kwa Wafanayakazi katika migodi hiyo ni muhimu pia. Walimshauri Mkurugenzi wa mgodi huo Bwana Steven Siame kuwa karibu na Taasisi za Serikali ili kuweza kufahamu mambo yote yanayotakiwa katika suala zima la uchimbaji ikiwemo Baraza la Usimamizi wa Mazingira kwa ajili ya kujua kanuni za utunzaji wa mazingira.

Ujumbe huo kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais upo katika ziara ya kutembelea migodi midogo inayomilikiwa na Wachimbaji wadogo kwa ajili ya kujifunza na kuona shughuli hizo za Uchimbaji zinavyofanyika katika migodi hiyo likiwemo na suala la utunzaji wa Mazingira kwa ujumla.
Mkurugenzi wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga wakiangalia mashine ya kuingia shimoni inayotumiwa na Wachimbaji wadogo wa mgodi wa Igulubi ulioko katika wilaya ya Igunga mkoani Tabora.
Mkurugenzi wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga wakionyeshwa na Afisa madini kanda ya Taabora Injinia Kasweke aina za mawe yenye dhahabu yanayopatikana katika Mgodi mdogo wa Igulubi wilayani Igunga mkoa wa Tabora.
Mkurugenzi wa sera na Mipango toka Ofisi ya Makamu wa Rais Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga na Afisa Mazingira Bi Suzan Nchala wakiangalia sehemu ambapo mawe yaliyopondwa husafishwa ili kupata dhahabu walipotembelea mgodi wa Igulubi wilayani Tabora.
Mmiliki wa mgodi mdogo wa Igulubi Bwana Steven Siyame akiwaonyesha wajumbe toka Ofisi ya Makamu wa Rais waliofanya ziara katika mgodi huo uliopo Igunga Tabora jinsi mashine ya kuvunjia mawe inavyofanya kazi( haipo pichani)

No comments: