Katika ulimwengu wa uchangamano, ufikivu wa habari ni muhimu katika kujenga
jamii yenye maarifa, iliyo shirikishi na endelevu. Huu ndio ujumbe wa Siku ya
Kimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote (IDUAI), ukizingatia jukumu muhimu ambalo
ufukivu wa habari hufanya katika kuendeleza Agenda ya 2030 ya Maendeleo
Endelevu.
Ufikivu habari ni haki ya msingi. Inawawezesha wanawake na wanaume kuelewa
na kushiriki katika kujenga na kushirikiana ujuzi wanaohitaji ili watoe mchango
kikamilifu katika jamii yao. Raia wenye taarifa sahihi huifanya serikali iwajibike.
Ufikivu Habari ni dereva wa uvumbuzi na ubunifu, kuongeza fursa kwa wote, hasa
kwa wasichana na wanawake.
Ufikivu habari huanza na kujitolea kwa Serikali kutengeneza, kueneza na
kutekeleza sera na sheria zinazohusu haki ya habari na kuhakikisha kuheshimiwa
kwa haki hii ya kibinadamu. Hii inahitaji utaratibu wa ufanisi wa utekelezaji na
utamaduni wa uwazi katika aina zote za taasisi. Wananchi wanahitaji pia kuwa na
fikra pana, ujuzi wa kusoma na ujuzi wa kidigitali ambao
unahitajika kufikia,
kuchambua na kutumia habari kwa njia tofauti, nje na ndani ya mitandao. Hii ndiyo
maana UNESCO inaziomba serikali zote na washirika kutumia uwezo wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano ili kusaidia kufikia Lengo la 4, Elimu Endelevu inayolenga kuhakikisha "elimu shirikishi, sawa na ya ubora na kukuza fursa za elimu isiyo na mwisho kwa wote; Ufikivu wa Habari pia unajumuisha kukuza uandaaji wa maudhui yanayofaa, yenye kulenga jamii husika na yanayopatikana kwa lugha mbalimbali. Yote hii inahitaji sera zenye ufanisi na ushirikiano mzuri katika ngazi zote.
Siku ya Kimataifa ya Ufikivu Habari kwa Wote pia ni fursa ya kurejea ahadi yetu ya
uhuru wa kujieleza na usalama wa waandishi wa habari. Vyombo vya habari
huchukua nafasi muhimu katika kuwezesha ufikivu wa habari kwa wananchi na
katika kufuatilia masuala muhimu ya kijamii na wakati huo huo vikiwaelimisha
wafuatiliaji kwa kuwapa ufahamu na ujuzi. Haiwezekani kuwepo kwa ufikivu wa
habari kwa wote bila kuwepo kwa vyombo vya habari vilivyo huru.
Ufikivu wa habari sio tu ni lengo peke yake; pia ni mchangiaji muhimu katika
utekelezaji wa malengo mengine yote ya Maendeleo Endelevu. Kwa hiyo ni
muhimu tuendeleze juhudi zetu ili kuhakikisha kuwa kila mwanamke na
mwanamume wanafurahia ufikivu kamili wa habari.
No comments:
Post a Comment