Ujumbe kutoka Ofisi yaMakamu wa Rais ukiongozwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji wakimsikiliza Mmiliki wa Mgodi wa Sambaru uliopo wilayani Ikungi Mkoani Singida, Bwana Yusuf Mwandami walipofanya ziara ya kutembelea mgodi huo.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais,Bi Magdalena Mtenga akiuliza swali kwa mmiliki wa mgodi wa sambaru uliopo Ikungi Mkoani Singida mara baada ya ujumbe toka Ofisi ya Makamu wa Rais kutembelea mgodi huo wa mwisho katika picha ni Afisa madini kanda ya Singida aliyeongozana na ujumbe huo Bi. Sofia Omary.
Mmiliki wa Mgodi mdogo wa dhahabu wa Sambaru uliopo Ikungi Bwana Yusuf Mwandami akitoa maelekezo kwa ujumbe huo juu ya mashine mbalimbalimbali zilizofungwa mgodini hapo zitakavyokua zinafanya kazi. Wa kwanza kulia ni Afisa madini kanda ya Singida aliyeongozana na ujumbe huo Bi. Sofia Omary.
Ujumbe kutoka Ofisi ya Makamu wa rais ukiongozwa na Mkurugenzi wa sera na Mipango Bi Ogenia Mpanduji pamoja na Mkurugenzi Msaidizi-Mazingira Bi. Magdalena Mtenga wakipata maelezo juu ya uendeshaji wa mgodi mdogo wa dhahabu ulioko Ikungi Bwana Ahmed Magoma.
Mkurugenzi Msaidizi Idara ya Mazingira Bi Magdalena Mtenga (wa kwanza kulia) akimuuliza maswali Mmiliki wa mgodi mdogo wa dhahabu ulioko Ikungi mkoani Singida Bwana Ahmed Magoma wakati ya ziara ya Ujumbe toka Ofisi ya Makamu wa Rais ilipotembelea mgodi huo.
No comments:
Post a Comment