Advertisements

Friday, September 15, 2017

Waliokamatwa na mzigo wa almasi JNIA wafikishwa Mahakamani Kisutu

Watuhumiwa waliokamatwa na mzigo wa almasi zenye thamani ya Sh 32.3 bilioni katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere(JNIA), wamefikishwa mahakamani Kisutu asubuhi leo Ijumaa.
Watuhumiwa hao walikamatwa na mzigo huo ambao ulizuliwa na Serikali ili ufanyiwe tathimini upya kujua thamani halisi baada ya thamani iliyotumika kutiliwa mashaka na Serikali.
Jeshi la polisi liliwashikilia watuhumiwa wanne kwa uchunguzi na hatua nyingine za kisheria baada ya kuzuia mzigo huo.
Mzigo huo wa almasi ulikuwa unatoka mgodi wa Mwadui ambao ni wa ubia kati ya Serikali na kampuni ya Petra Diamonds ya Afrika Kusini kwa hisa 25 za Serikali na Petra Diamonds hisa 75.

Chanzo: Mwananchi

No comments: