ANGALIA LIVE NEWS

Saturday, September 23, 2017

WAZIRI CHARLES MWIJAGE AFUNGUA TAWI LA KAMPUNI YA MABATI ALAF DODOMA

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage akifungua tawi la kampuni ya mabati ya ALAF Dodoma. Kushoto ni meneja mkuu Upauaji (roofing) wa Kampuni ya mabati ALAF, Dipti Mohanty akishuhudia ufunguzi huo. 

WAZIRI wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Bw. Charles Mwijage Septemba 9, 2017 alifungua tawi la Kiwanda cha mabati ALAF katika mkoa wa Dodoma eneo la Kizota kitalu namba 148.

Kufunguliwa kwa tawi hili katika mkoa wa Dodoma ni kutokana na maamuzi ya serikali kuamia makao makuu ya nchi mkoani Dodoma kwa vitendo na kuunga mkono kauli mbiu ya Mheshimiwa Rais John Magufuli katika “ USHIRIKI KATIKA KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA TAIFA”.

Kufunguliwa kwa tawi hili kutaimarisha maendeleo ya mkoa wa Dodoma na maeneo ya jirani.

Wateja kutoka Dodoma na Singida sasa wataweza kupata suluhisho la mahitaji ya bidhaa za uezekaji kutola ALAF.

Tunauza bidhaa zilizo tayari kwa matumizi kulingana na mahitaji ya mteja hasa mabati ya rangi pamoja na kutoa ushauri wa kiufundi na kiutaalamu.

Kwa sasa kiwanda chetu cha ALAF kina matawi manne Mbeya, Mwanza, Arusha na Dodoma.

Kuhusu kampuni ya ALAF

Kampuni ya ALAF ni sehemu ya kampuni ziliyoko chini ya Kampuni ya SAFAL, kampuni inayoongoza bila mpinzani ktika utoaji wa bidhaa bora za uezekaji barani Afrika.Kampuni ya SAFAL inaendesha shughuli zake katika nchi 13 kuanzia mashariki,kati na kusini mwa bara la Afrika.

Tukiwa na uzoefu wa zaidi ya miaka 50 katika biashara, ALAF tunaongoza katika uzalishaji wa bidhaa za uezekaji za chuma.Katika kuongezea bidhaa zake za upauaji, bidhaa za kitaalamu pia zinauzwa na ALAF kama misumari (fixtite fastener), steel pipes, na Hollow section pamoja na viambatanisho muhimu kwa uezekaji.

Baadhi ya bidhaa zinazotolewa na ALAF ni Lifestile, Romantile, Versatile, Tekdek (It5), Resincot na Simba Dumu.

Wasilana nasi kwa namba hizi Dar es Salaam- O768 555 560, Arusha - 0763 707 071, Mbeya - 0765 555 560, Dodoma - 0764 131442 na Mwanza 0682 808 080.

Tunapatikana pia kuitia mitandao ya kijamii Facebook -Alaf Limited na Instagram - Alaf Limited

No comments: