Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi akizungumza na washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni na Ubungo. Kulia ni Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo.
Mwenyekiti wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Saida Mukhi (kulia) akizungumza na washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia.
Ofisa Mradi wa Kituo cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC, Suzan Charles akitoa ufafanua juu ya mradi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa
Dar es Salaam.
Mmoja wa washiriki wa warsha hiyo kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi akichangia mada.
KITUO cha Usuluhishi wa masuala ya kijamii na kijinsia, CRC kimezinduwa mradi wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, yaani Kinondoni na Ubungo.
Akizungumza na wadau wa mradi huo yaani baadhi ya wasaidizi wa sheria, maofisa ustawi wa jamii, wanasheria, mahakimu, Askari Polisi Dawati la Jinsia, maofisa watendaji wa mitaa kutoka wilaya za Kinondoni na Ubungo, Mwenyekiti wa CRC, Saida Mukhi aliwataka wadau hao kushirikiana ili kuhakikisha vitendo vya ukatili wa kijinsia vinakomeshwa na kupungua.
Alisema lengo la mradi huo unaofadhiliwa na shirika la Legal Service Facilities (LSF) ni kuhimarisha zaidi upatikanaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa ukatili wa kijinsia. Aliongeza kuwa mradi huo utajikita zaidi katika utoaji wa msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa waathirika na kuhakikisha mfumo wa upatikanaji wa haki unafanya kazi vizuri.
"...wadau katika maeneo hayo mnatakiwa kuhakikisha tunapinga vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo vinaweza kusababisha madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii, ikiwa ni pamoja na wahusika kunyimwa uhuru," alisema Bi. Saida Mukhi akifungua warsha ya wadau hao.
Kwa upande wake, Mratibu wa Kituo cha Usuluhishi cha CRC, Bi. Gladness Munuo akifafanua zaidi kwa washiriki wa semina hiyo alisema mradi huo utaendeshwa katika Kata za Makumbusho na Kawe kwa Wilaya ya Kinondoni huku kwa Wilaya ya Ubungo utajikita kwenye Kata ya Saranga.
Alisema CRC itashirikiana na wadau katika maeneo hayo kuhakikisha inapiga vita vitendo vya ukatili wa kijinsia ambavyo mara nyingi vimekuwa na madhara ya mwili, kingono au kisaikolojia au mateso kwa wanajamii na mara nyingine kuwanyima uhuru. Sehemu ya washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni (Kata za Makumbusho na Kawe) na Ubungo (Kata ya Saranga).
Sehemu ya washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia kwenye wilaya mbili za mkoa wa Dar es Salaam, Kinondoni (Kata za Makumbusho na Kawe) na Ubungo (Kata ya Saranga).
Picha ya pamoja ya washiriki wa warsha kwa wadau wa utoaji wa huduma za msaada wa kisheria na ushauri nasihi kwa wahanga wa vitendo vya ukatili wa kijinsia wakiwa na mgeni rasmi Bi. Saida Mukhi.
No comments:
Post a Comment