Na
Yeremias Ngerangera, Namtumbo
Athmani Amani mkazi wa kijiji cha Naikesi kata ya kitanda wilayani Namtumbo mkoani Ruvuma anawaomba watanzania kumsaidia fedha za kugharimia matibabu ya mtoto wake Shaziri Athmani (12) anayesumbuliwa na tatizo la moyo kuwa mkubwa.
Mtoto Shaziri Athamani ni mwanafunzi wa darasa la nne shule ya msingi Naikesi iliyopo kata ya Kitanda wilayani Namtumbo awali alikuwa anasumbuliwa na kuvimba miguu hali iliyokuwa inamkosesha masomo yake darasani mara kwa mara kuanzia mwaka 2016.
Mwaka huo huo mwezi Septemba baba yake alilazimika kumpeleka Hospitali ya Mkoa Songea kuangalia tatizo la kuvimba kwa miguu ya mtoto huyo na baada ya kupata vipimo wakashauriwa kuenda Hospitali ya Peramiho .
Bwana Athamani alidai kuwa hakuwa na fedha za kumpeleka mtoto peramiho kwa kipindi hicho na badala yake alirudi naye nyumbani Naikesi kwenda kuuza mifugo lakini fedha hizo hazikumwezesha kukidhi mahitaji ya kumtibu mwanoa katika Hospitali ya Peramiho baada ya kufika katika Hospitali hiyo na kumaliza fedha yake yote aliyokuwa nayo katika vipimo pekee .
Baada ya kupatiwa vipimo na kubaini Tatizo la mwanae alirudi na mwanae mpaka kijijini kwake kujipanga upya kwa ajili ya matibabu ya mwanae na kujitahidi kwa kile anachokipata anunue dawa kwa ajili ya mwanae huyo.
Pamoja na jitihada hizo hali ikaendelea kuwa sio nzuri na ndipo alipolazimika kufanya kazi za kulima mashamba ya watu ili apate fedha za kumtibu kijana wake na mwaka huu mwezi oktoba alimpeleka kijana wake huyo peramiho na baada ya kufika peramiho na kupatiwa vipimo alishauriwa na madaktari kumpeleka mtoto huyo Hospitali ya Muhimbili Dar es Salaam.
Hata hivyo mzazi huyo alifika katika ofisi ya Katibu tawala wa wilaya ya Namtuimbo na kufanya mazungumzo na Kaimu katibu tawala wa wilaya ya Namtumbo Alkwin Ndimbo kwa lengo la kupatiwa msaada wa matibabu wa kijana wake huyo.
Alkwin alidai kuwa kuna sababu ya watanzania wenye moyo kumsaidia mtoto huyo kwa michango yao ili mzazi wa kijana huyo aweze kumpeleka kijana wake huyo Hospitali ya Taifa Muhimbili na bila michango kutoka kwa watanzania wenye moyo mzazi huyo hana uwezo wa kumpeleka kijana wake huyo Hospitali ya Taifa Muhimbili.
Kwa watanzania wenye moyo wa kumsaidia mtoto huyo wanaweza kumpigia mzazi wake kupitia namba 0629629872 au unaweza kumtumia fedha kupitia namba hiyo ambapo kwa sasa mzazi huyo amerudi kijijini kwake Naikesi akiwa na mgonjwa wake akihangaika kupata fedha za kumpeleka mtoto wake huyo Hospitali ya Taifa Muhimbili.
No comments:
Post a Comment