ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 9, 2017

BENKI YA CRDB YACHANGIA UJENZI WA VYOO WILAYANI CHATO.

Meneja wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus, akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi vifaa hivyo katika halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita.

Walioketi ni Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas (katikati) pamoja na Mkurugenzi wa huduma kwa wateja wakubwa Goodluck Nkini, aliyemwakilisha Mkurugenzi Mtendaji CRDB.

Na Binagi Media Group
Katika kuadhimisha wiki ya huduma kwa wateja, benki ya CRDB imechangia vifaa vya ujenzi wa vyoo katika shule za halmashauri ya wilaya ya Chato mkoani Geita ili kusaidia utatuzi upungufu wa vyoo katika shule za halmashauri hiyo.

Mkurugenzi wa CRDB tawi la Mwanza, Wambura Calystus alisema vifaa hivyo vitasaidia ujenzi wa vyoo katika shule za msingi za Kalema, Muungano na Katemwa A na kwamba vifaa hivyo vimejumuisha mifuko 150 ya theruji, mabati, sinki za vyoo pamoja na vyombo vya kukusanyia taka na tenki la maji kwa ajili ya halmashauri ya Chato.

Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas aliishukuru benki hiyo na kubainisha kwamba bado kuna uhaba wa vyoo kwenye shule nyingi na kuiomba kuendelea kusaidia utatuzi wa changamoto hiyo ili kutoa chachu kwa wadau na benki nyingine kuiga mfano huo.

Zoezi la kukabidhi vifaa hivyo lilifanya ijumaa Oktoba 06,2017 katika halmashauri ya wilaya ya Chato ikiwa ni muda mfupi baada ya benki ya CRDB kutoa semina kwa wateja wake wilayani humo na pia kutoka maeneo jirani ikiwemo Muleba, Katoro na Biharamulo.

Meneja wa CRDB tawi la Chato, Msigwa Mganga, akizungumza kwenye zoezi la kukabidhi vifaa hivyo.
Zoezi la kukabidhi vifaa vya ujenzi wa vyoo katika shule za halmashauri ya Chato.
Kaimu Mkurugenzi wa halmashauri ya Chato, Mwl.Delphina Cosmas (wa pili kushoto) pamoja na viongozi wengine wakipokea vifaa hivyo.

No comments: