Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ambaye alikuwa Mgeni Rasmi akifungua Kongamano la walimu na Benki ya NMB ambalo limefanyika kwa mala ya kwanza Mkoani Geita.
Meneja wa Benki ya NMB Mkoani Geita Mathias Nkuliwa akizungumza wenye Kongamano hilo ambapo alisema lengo la kungamano hilo ni kutambua mchango wa walimu katika Benki ya NMB.
Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga Akizungumza na walimu wakati wa Kongamano ambalo limeandaliwa na NMB Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita. Baadhi ya walimu ambao wanatoka kwenye halmashauri zilizopo Mkoani Geita wakifuatilia Hotuba ya Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga.[/caption] UTAFITI nchini Tanzania unaonesha kuwa bado kuna idadi kubwa ya Watanzania ambao hawatumii mfumo rasmi wa uifadhi fedha kibenki kutokana na kukosa elimu za kibenki. Utafiti unaonesha ni zaidi ya asilimia ishirini (20) tu ndio wanaotumia huduma za kibenki. Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga alipokuwa kwenye Kkongamano la Siku ya Walimu, kwa kusisitiza ipo haja ya mabenki na taasisi nyingine za kifedha kuwa na program maalumu za utoaji elimu ya masuala ya kifedha hususani maeneo ya vijijini. “Hivyo basi kuna kila sababu ya kuvishauri vyombo vya fedha na taasisi nyingine husika kuwa na program maalumu za kutoa elimu ya masuala ya kifedha hususani maeneo ya vijijini ili watanzania walio wengi zaidi waweze kunufaika na maendeleo yaliyofikiwa na sekta ya fedha hapa nchini,” alisema Kyunga. Naye Mkuu wa Kitengo cha Biashara kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa Benki ya NMB, Omar Mtiga alisema idadi ya Watanzania kwa sasa ni takribani milioni 50, huku asilimia 20 tu kati yao ndio wenye akaunti za benki, ilhali zaidi ya asilimia 60 ya wananchi wanamiliki simu za mkononi na wana uwezo wa kufanya malipo na miamala kupitia simu za mkononi. “NMB kwa sasa inaamini katika kutoa huduma za kibenki za kidigitali kwa watanzania wote, njia hii tunaiona ni bora zaidi na inaendana na kasi ya ukuaji wa teknolojia na itasaidia kuleta mwamko mkubwa zaidi kwa watanzania wengi kuweza kutumia huduma za kibenki kwa kufanya miamala na malipo mbali mbali,” alisema Mtinga. Mtinga ameendelea kuelezea kuwa wateja walionao ni zaidi ya milioni 2.5 kati yao zaidi ya wateja milioni 2 wanatumia simu za mkononi kufanya miamala na kuangalia salio ,kufanya malipo mbalimbali kama kulipia umeme hata kulipia kodi mbalimbali. Picha/MADUKA ONLINE
No comments:
Post a Comment