Makamu wa Rais wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania (TAT), Omar Kiponza akizungumza na vyombo vya habari kuelezea kero mbalimbali zinazowakabili wanachama wake leo katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania (TAT), Omar Kiponza akizungumza na vyombo vya habari kuelezea kero mbalimbali zinazowakabili wanachama wake leo katika ofisi za chama hicho jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Ofisa Mwendeshaji Mkuu wa chama hicho, Hussein Wandwi.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam Makamu wa Rais wa Chama cha Wasafirishaji Tanzania (TAT), Omar Kiponza alisema baadhi ya barabara ambazo magari ya wanachama wao wamekuwa wakipita kila siku hakuna sehemu maalum ya maegesho hivyo utaratibu unaotumiwa kuvuta magari bila ridhaa yanapokamatwa sio wa kiungwana hivyo kushauri mamlaka husika kukutana na viongozi wa TAT kupata suluhu la suala hilo.
"...wamekuwa wakivuta magari bila kutaka maelezo hata kama gari linaweza kutembea lenyewe na kosa kubwa wanalosema ni kwamba umepaki kwenye road reserve hata kama dereva amesimama kwa ajili ya dharura ya posho au document wanakuambia gari iondolewa iende misugusugu na fine wanazotoza huwa ni kubwa mno. Ikiwa mwanachama wetu atafanya gereji Barabarani au kufunga njia kwa uzembe basi hapo hatuna pingamizi lolote sheria ifuate mkondo wake na hatuwezi kutetea uharibifu wa miundombinu ya nchi yetu," alisema Omar Kiponza.
Alisema kutokana na suala la mkanganyiko wa uzidishaji mzigo wameiomba TANROADS kuweka mzani bandarini kama walivyoomba awali ili kuondoa mkanganyiko huu. Alisema gari linaweza kupima mizani miwili na kuonekana lipo sahihi lakini likifika mzani wa tatu linaambiwa limezidisha na kutozwa faini jambo ambalo ni utata mkubwa.
"...Kuna suala la mizani kutofanyiwa 'calibration' hili suala limekuwa likizunguziwa kwa muda mrefu sana na mizani mingi haina uwiano katika usomaji, tunawaomba muliangalie suala hili kwa umakini ili sote tufanye kazi kama marafiki.
Upande wa mamlaka ya mapato Tanzania yaani TRA pia kumekuwa na kero ambayo wanachama wetu wanapenda kutoa malalamiko hii ni juu ya suala la utozaji wa faini ya shilingi elfu 40,000 endapo gari litakuwa halijavuka mpaka ndani ya siku7 pale tunduma,"
Aidha alisema kero nyingine ni kwa mamlaka ya SUMATRA ambapo imekuwa ikitoza wanachama wao gari la mzigo ambalo halifanyi kazi tangia linunuliwe kwa madai ni utaratibu, jambo ambalo wanaamini ni uonevu.
"Unakuta ulinunua gari la mizigo bovu au lilisimama kufanya kazi kwa miaka ukienda kuomba leseni ya usafirishaji unatozwa faini kwa kitu ambacho hakijawahi kutembea kwa kisingizio kuwa faini hiyo ni kwa ajili ya part registration sasa faini ya nini kwa kitu ambacho hakijatumika?
"Vivyo hivyo kuna jambo lingine linalohusisha watu wa maliasili pindi magari yanapopakiwa mkaa na madereva siyo kwa ruhusa ya tajiri lakini wanapokamatwa adhabu yote ya faini analipishwa tajiri wakati huo huo dereva hapewi adhabu yoyote je hii ni sawa kweli,kwa sababu kuna wasafirishaji ambao washapigwa faini kama milioni 24 kwa sababu ya mkaa je mamlaka husika wanafahamu hili au ni sheria watu wanajichukulia mikononi.
No comments:
Post a Comment