Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akizungumza wakati wa kikao cha kazi na Wakuu wa Idara na Vitengo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa wizara ya Kilimo (Kilimo IV)
Wakuu wa Idara na Vitengo wakimsikiliza kwa makini Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) wakati wa kikao cha kazi kwenye Ukumbi wa Mikutano wa wizara ya Kilimo (Kilimo IV)
Kikao kikiendelea
Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe akizungumza wakati wa kikao cha kazi kilichoongozwa na Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb)
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) (Kushoto) na Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe wakifatilia kikao cha kazi kilichowakutanisha na Wakuu Idara na Vitengo
Mkurugenzi wa Idara ya Maendeleo ya Utafiti Dkt Mansoor Hussein
Picha ya pamoja Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) (Katikati), Katibu Mkuu wa Wizara ya kilimo Mhandisi Mathew John Mtigumwe na wakuu wa Idara na Vitengo mara baada ya kumalizika kwa kikao cha kazi.
Mkurugenzi wa Utawala na rasilimali watu wa Wizara ya Kilimo Ndg Seushi Mburi akisoma taarifa fupi ya Wizara ya kilimo
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa (Mb) akitafakari jambo wakati kikao kikiendelea
Na Mathias Canal, Dodoma
Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa leo Octoba 26, 2017 amewaagiza watumishi kutofanya kazi kwa mazoea badala yake kuongeza ufanisi katika kazi kwa kuwa wabunifu, na waadilifu.
Mhe Naibu Waziri ametoa agizo hilo wakati wa kikao cha kazi alipokuwa akizungumza na Wakuu wa Idara na Vitengo wa wizara hiyo kwenye Ukumbi wa Mikutano wa wizara ya Kilimo (Kilimo IV), kwa lengo la kufahamiana na kujua majukumu ya kila idara na vitengo.
Alisema kuwa ili kutimiza adhma ya serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe Dokta John Pombe Magufuli katika kuboresha huduma za wananchi ni lazima watumishi kubadili taswira ya kufanya kazi kwa mazoea na kuhamia kwenye kasi ya viwango yakinifu na weledi.
Mhe Mwanjelwa alisema kuwa Wakuu hao wa Idara na Vitengo wanajukumu kubwa la uwakilishi wa watumishi wenzao 1828 wanaohudumu katika Wizara ya kilimo kote nchini hivyo ili kuwafanya wananchi kubadili mbinu za kilimo kutoka kilimo kwa ajili ya chakula pekee hadi kufikia kilimo kwa ajili ya chakula na biashara ni lazima watumishi wote kuwa wabunifu na kutumia taaluma zao kwa manufaa ya wananchi na Taifa kwa ujumla.
Katika kikao hicho kilichoongozwa na Naibu Waziri Mhe Dkt Mary Machuche Mwanjelwa Kilihudhuriwa na Mkuu wa Idara ya Utawala na Rasilimali watu, Sera na Mipango, Mafunzo, Zana za kilimo, Utafiti na Maendeleo, Usalama wa Chakula, Maendeleo ya mazao na Matumizi bora ya Ardhi.
Wengine ni Wakuu wa Vitengo; Kitengo cha Fedha na Uhasibu, Kitengo cha Ukaguzi wa ndani, Kitengo cha Habari na Mawasiliano serikalini, Kitengo cha sheria, Kitengo cha Ugunduzi na Ugavi na Kitengo cha TEHAMA.
“Kubwa na la msingi ambalo ningependa kuwaasa na ninyi kukumbuka kuwa hii ni awamu ya tano ya kazi na mchakamchaka, hivyo badilisheni Mindset ili tufanye kazi kwa kumsaidia Rais kwa weledi, ubunifu, Maarifa, Juhudi na uzalendo, bado kuna watu wanatembea badala ya kukimbia’’
“Ni lazima tukimbie lakini uwe mchakamchaka with Quality kwani watu wanaamini katika matokeo chanya, kwahiyo kuanzia sasa ni lazima tukimbizane na kasi ya awamu ya tano kwa kuongeza ufanisi kwenye wizara ya kilimo na business As Usual ni Marufuku” Alikaririwa Mhe Mwanjelwa
Mhe Naibu Waziri Dkt Mwanjelwa alisema kuwa wataalamu wanapaswa kutumia utaalamu wao na kuonyesha matokeo chanya kwani kufanya hivyo kutaongeza imani kubwa kwa serikali inayotekeleza ilani ya ushindi ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi CCM.
Aliongeza kuwa Kilimo ni uti wa mgongo kwani zaidi ya asilimia 75 ya wananchi ni wakulima ambapo mtaji wake ni nguvu na ardhi hivyo wasiposaidiwa kuboresha kilimo chao na kuongeza uzalishaji ni wazi kuwa Taifa litaendelea kusalia nyuma kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment