Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa na viongozi wa Jeshi la Polisi Sambamba na Askari Polisi walioshiriki na kujinyakulia medali mbalimbali katika mashindano ya mchezo wa Taekwondo iliyo andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association)
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simon Sirro, akiwa na askari wa jeshi hilo wanaounda timu ya Taekwondo ambao walishiriki na kujinyakulia medali mbalimbali katika mashindano ya Taekwondo yaliyo andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association) yaliyoshirikisha vilabu 17 vya Taekwondo kutoka nchi nzima.
Mkuu wa Jeshi la Polisi Nchini (IGP) Simoni Sirro akimvisha medali askari Polisi ambaye ni miongoni mwa askari waliojinyakulia medali katika mashindano taekwondo iliyo andaliwa na Ubalozi wa Jamuhuri ya Korea ukishirikiana na Chama cha walimu wa Taekwondo kutoka Korea. (Korean Taekwondo Masters Association). Picha zote na Jeshi la Polisi
Na Jeshi la Polisi
Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini IGP Simon Sirro amewataka Maofisa na Askari Polisi kote nchini kushiriki michezo ili kujenga Afya,ukakamavu na urafiki baina ya wenyewe kwa wenyewe na raia.
IGP Sirro ameyasema hayo jijini Dar Es Salaam wakati hafla fupi ya kuwapongeza wachezaji wa TAEKWONDO waliofanya vizuri katika michezo ya Taekwondo Pumsae (kucheza Kata), Taekwondo Gyeokpa ( kuvunja kibao kwa kuruka Juu) na Taekwondo Gyeorugi (Mapigano) iliyomalizika hivi karibuni ambapo timu ya Polisi iliibuka na ushindi wa kwanza katika timu 17 zilizoshiriki.
Sirro alisema Jeshi la Polisi litaendelea kutilia mkazo michezo ya aina mbalimbali na atahakikisha Askari na Maofisa wanapata fursa ya kushiriki michezo kwakuwa kwakufanya hivyo kutasaidia pia kulitangaza Jeshi la Polisi na kujenga mahusiano na jamii.
"Hakikisheni hamrudi nyuma,tutawapa sapoti ya kila namna ili tusiwe wasindikizaji bali tuweze kutoa ushindani na kufanya vyema na ni jambo linalowezekana kwa kuwa ari na morali ipo"Alisema Sirro.
Kwa Upande wake Mkuu wa Michezo wa Jeshi la Polisi,Kamishna Msaidizi wa Polisi ACP Philip Kalangi alisema ushindi wa timu hiyo ni chachu katika kujiandaa na michezo ya majeshi ya EAPCCO itakayofanyika hapa nchini mwakani ambapo Tanzania itakuwa mwenyeji.
mashindano hayo yaliyoandaliwa na ubalozi wa Jamhuri ya korea ukishirikiana na Chama cha Walimu wa Taekwondo kutoka korea (Korean Taekwondo Masters Association) ambayo ni mashindano ya Taekwondo ya kitaifa yaliyofanyika tarehe 21/10/2017 ambayo yalishilikisha vilabu 17 vya Taekwondo kutoka nchi nzima ambavyo ni Makongo Juu, Kariakoo,Shark TKD,Twiga Triple A,HTC DSM, KILI, Vingunguti,Arusha Morden,TCC,AICC,UAUT pamoja na vilabu vya Polisi ambavyo ni DPA, MPA na ZPA.
No comments:
Post a Comment