ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 9, 2017

IHEMBE MABINGWA KOMBE LA MBUNGE WA KARAGWE

 Mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa akimpokea mgeni rasmi Waziri wa Mambo ya Ndani Mh. Mwigulu Nchemba
 Mgeni rasmi akiwasili katika uwanja wa changarawe ilipofanyika fainali ya Bashungwa Karagwe Cup
 Mheshimiwa Mwigulu Nchemba akikagua vikosi vya Ihembe na Nyaishozi
 Mchezaji wa Ihembe akipiga mpira wa kona
 Uwanja wa Changarawe ulihosheheni mamia ya mashabiki wa mpira wa miguu
  Ihembe wakishangilia baada ya kupata bao la kwanza
 Wadau wakishuhudia mtanange toka jukwaa la “mzunguko”
 Wachezaji wa Ihembe wakiwa wamemzunguka golikipa wao baada ya kupata kash kash
 Mashabiki wa Nyaishozi wakifuatilia kwa makini mchezo wa Bashungwa Karagawe Cup
 Kombe likikabidhiwa kwa mgeni rasmi
Mbunge wa Karagwe Mh. Innocent Bashungwa akitoa neno la pongezi kwa timu zote shiriki
 Kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime akimkabidhi kombe nahodha wa Ihembe
 Ihembe wakifurahia kombe lao la ubingwa wa Bashungwa Karagwe Cup
Furaha na shangwe baada ya kutangazwa mabingwa

Timu ya kata ya Ihembe imeibuka mabingwa wa Bashungwa Karagwe Cup 2017 baada ya kuifunga Nyaishozi mabao 2-1. Mchezo huo uliopigwa katika uwanja wa Changarawe huku mgeni rasmi akiwa Waziri wa Mambo ya ndani Mheshimiwa Mwigulu Nchemba uliteka hisia za mamia ya wakazi wa jimbo la Karagwe waliojitokeza kwa wingi.

Ihembe walikuwa wa kwanza kupata goli dakika 25 kupitia kwa Athumani Chuji aliepiga shuti kali la mpira wa adhabu uliomshinda golikipa wa Nyaishozi na kuingia wavuni. Bao hilo lilionekana kuwachanganya Nyaishozi ambao walionyesha kutoelewana katika eneo la ulinzi na kujikuta wakiruhusu bao la pili katika dakika ya 35 lililofungwa na Mshauri Kato aliewatoka walinzi wa Nyaishozi na kufunga goli la kiustadi.  Kipindi cha pili Nyaishozi waliuanza mchezo kwa kasi na kufanikiwa kupata bao katika dakika ya  78 lililofungwa na mshambuliaji MC, hata hivyo jitihada za kusawazisha matokeo zilikwamishwa na mlinda mlango wa Ihembe alieokoa michomo mingi.

Kufuatia ushindi huo Ihembe walijipatia kombe na kiasi cha fedha shilingi milioni moja na nusu huku Nyaishozi wakipata shilingi laki saba na nusu kama kifuta jasho kwa kushika nafasi ya pili. Akizungumza baada ya mchezo huo mbunge wa Karagwe Mheshimiwa Innocent Bashungwa alisema mashindano hayo yatakuwa endelevu kila mwaka ili kuibua vipaji vya vijana wa Karagwe waweze kujiajiri kupitia michezo na kuahidi kuboresha mashindano yajayo kwa kusaka wadau wengine watakaohakikisha wilaya ya Karagwe inakuwa na timu bora ya kushiriki ligi kuu.

Nae kocha bora wa ligi kuu msimu uliopita ambaye pia ni kocha wa Kagera Sugar Meck Mexime aliyapongeza mashindano hayo na kuahidi mchezo wa kirafiki baina ya Kagera Sugar na  kikosi cha wachezaji bora waliochaguliwa toka mashindano hayo.

 

No comments: