ANGALIA LIVE NEWS

Monday, October 9, 2017

KAIMU MKURUGENZI RAHCO AFANYA ZIARA YA KUSHTUKIZA USIKU KATIKA MRADI WA RELI YA KISASA

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (wa pili kulia) akiongozwa na  Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi (kushoto) pamoja na Meneja mradi huo kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya YAPI Merkezi kutoka Uturuki, Abdullah Milk mara baada ya kufika eneo la Soga - Kibaha jumamosi usiku kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.
 Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi akitoa ufafanuzi juu ya mradi.
 Watanzania waliopata nafasi ya kufanyakazi katika mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge wametakiwa kufanya kazi kwa uweledi na kuacha ubabaishaji.

Ujumbe huo aliutoa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa wakati alipofanya ziara ya kushtukiza usiku wa jumamosi katika kambi mbalimbali za mradi huo zilizopo Pugu mpaka eneo la Soga Kibaha ili kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.

Kadogosa alisema mradi huo unatakiwa kwenda kwa kasi na kukamilika haraka hata kabla ya muda husika hivyo kila mtu atakayefanya kazi katika mradi huo anakikishe anafanya kazi na sio ubabaishaji utakaopelekea mradi huo kuchelewa.

Aidha Kadogosa alisema wamefikia makubaliano ya kufanya kazi usiku na mchana ili kuharakisha mradii huo na wakandarasi wanafanya haraka na kwa ukubwa wa mradi huu ni lazima tufanye kazi usiku na mchana.

“Kama mnakumbuka wakati Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Makame Mbarawa alipokuja hapa alisema ni lazima twende kasi na wakandarasi wetu wameamua kwenda na kasi na sasa mnaona tuta linaendelea vizuri ni lazima mradi huu ufanywe usiku na mchana kutokana na ukubwa wake,”alisema.
 Msafara huo ulipofika eneo la mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge Soga - Pwani.
 Shughuli ya ujenzi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge Soga - Pwani ikiendelea.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni Hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO), Masanja Kadogosa (wa kwanza kulia) akiongea machache na makandarasi wa mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge wakati alipofanya ziara ya kushtukiza katika kambi mbalimbali za mradi huo zilizopo Pugu mpaka eneo la Soga -Kibaha ili kuona endapo wakandarasi wa mradi huo wanafanya kazi usiku na mchana kama walivyosema katika mkataba wao na serikali.
 Meneja Mradi wa reli ya Kisasa ya Standard gauge kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi akitoa ufafanuzi juu ya mradi. Kwa upande wake Meneja Mradi huo kutoka RAHCO, Maizo Mgedzi alisema kazi inayoendelea kwa sasa ni kuendelea kusawazisha tuta ikiwa ni pamoja na kukata na kujaza, kujenga mifereji na madaraja ya reli pamoja na kuweka miundombinu ya umeme pamoja na vifaa vya kuongozea reli.

“Kazi imeanzia kilometa sifuri kutoka Dar es Salaam kwa sasa hivi wakandarasi wanaendelea kazi ya tuta kukata na kujaza wana mitambo zaidi ya 106 na kazi kubwa ni kujenga tuta wanaendelea vizuri ili kuhakikisha wanakwenda kwa kasi inayotakiwa,”alisema Magedzi.
Kwa upande wake Meneja mradi kutoka kampuni inayotekeleza mradi huo ya YAPI Merkezi kutoka Uturuki, Abdullah Milk alisema kampuni hiyo imejipanga kuhakikisha mradi huo unatekelezwa usiku na mchana ili kuhakikisha mradi unakamilika kwa wakati.

No comments: