Utafiti
uliofanywa na Shirika la hutetea haki za watoto wafanyakazi wanyumbani WOTESAWA
Jijini Mwanza, unaonyesha kwamba watoto hao bado wanakumbana na aina mbalimbali
za ukatili ikiwemo utumikishwaji.
Utafiti huo
uliofanyika mwaka jana ulibaini kwamba asilimia 91.9 ya watoto wafanyakazi wa
nyumbani katika Kata nne za Jiji hilo hawana mikataba ama makubaliano baina ya
wazazi na waajiri wao, asilimia 5.4 wana mikataba huku asilimia 80 ikionyesha
wapo wanaofanya kazi bila malipo huku wanaolipwa mshahara chini ya shilingi
20,000 wakiwa ni asilimia 20.
Utafiti huo
ulifanyika katika Kata za Igogo ambapo watoto wafanyakazi wa nyumbani 43
walifikiwa, Mkuyuni 42, Nyamagana 32 pamoja na Butimba 37 na hivyo kufanya
idadi ya watoto wafanyakazi wa nyumbani waliofikiwa kuwa 154, wavula wakiwa ni
16 na wasichana 138.
Hali hii
inaongeza chachu kwa shirika la WOTESAWA kuwajengea uwezo watoto wafanyakazi wa
nyumbani, waajiri wao pamoja na viongozi mbalimbali wakiwemo Madiwani,
Watendaji, Wenyeviti wa Mitaa, Maafisa Ustawi wa Jamii, pamoja na maofisa wa
dawati la jinsia kutoka jeshi la polisi kama anavyoeleza Mkurugenzi wa shirika
hilo, Angel Benedicto.
Washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza Mkurugenzi wa WOTESAWA, Angel Benedicto
Mkurugenzi wa WOTESAWA, Angel Benedicto akizungumza kwenye semina hiyo
Washiriki wa semina hiyo wakimsikiliza Mratibu wa Shirika la WOTESAWA
Mratibu wa Shirika la WOTESAWA, Elisha Daud akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Mratibu wa Shirika la WOTESAWA, Elisha Daud akiwasilisha mada kwenye semina hiyo
Mmoja wa washiriki wa semina hiyo akiandika maazimio
Washiriki wa semina hiyo
Diwani wa Kata ya Butimba, John Pambalu akitoa salamu za shukurani wakati wa tamati ya semina hiyo
Washiriki
Ukumbi wa pili, semina kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani pamoja na waajiri wao
Semina kwa watoto wafanyakazi wa nyumbani pamoja na waajiri wao
Picha ya pamoja
Bonyeza HAPA uchaguzi wa viongozi wa watoto wafanyakazi wa nyumbani
No comments:
Post a Comment