ANGALIA LIVE NEWS

Thursday, October 12, 2017

MASAUNI ALITAKA JESHI LA ZIMAMOTO KUFUNGUA VITUO WILAYA ZOTE NCHINI

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Makamishna na Wakuu wa Vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Masauni alilitaka Jeshi hilo kutoa elimu zaidi kwa umma pamoja na kuongeza kasi ya ufunguaji wa vituo vya zimamoto katika wilaya zote nchini. Kushoto ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, (CGF), Thobias Andengenye, na kulia ni Kamishna wa Utawala na Fedha wa Jeshi hilo, Michael Shija. Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF), Thobias Andengenye akitoa taarifa yake utendaji kazi wa Jeshi lake kwa Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (katikati meza kuu), wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsikiliza Mchumi wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, Boniface Mkumbo alipokua anafafanua mipango mbalimbali ya kuliendeleza jeshi hilo. Kulia kwa Naibu Waziri ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, (CGF), Thobias Andengenye. Katika hotuba yake kwa viongozi wa Jeshi hilo, Masauni alilitaka Jeshi hilo kutoa elimu zaidi kwa umma pamoja na kuongeza kasi ya ufunguaji wa vituo vya zimamoto katika wilaya zote nchini.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni akizungumza na Makamishna na Wakuu wa Vitengo vya Jeshi la Zimamoto na Uokoaji wakati alipofanya ziara Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo. Katika hotuba yake Masauni alilitaka Jeshi hilo kutoa elimu zaidi kwa umma pamoja na kuongeza kasi ya ufunguaji wa vituo vya zimamoto katika wilaya zote nchini. Kulia kwa Naibu Waziri ni Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, (CGF), Thobias Andengenye.
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni (kulia) akimsalimia Kamishna Jenerali wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji, (CGF), Thobias Andengenye, wakati kiongozi huyo alipofanya ziara ya kikazi Makao Makuu ya Jeshi hilo, jijini Dar es Salaam leo.

Na Felix Mwagara (MOHA)
NAIBU Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amelitaka Jeshi la Zimamoto na Uokoaji kuongeza kasi kufungua vituo vya zimamoto katika wilaya zote nchini pamoja na kutoa elimu kwa umma juu ya kinga na tahadhari ya majanga ya moto
Akizungumza na Makamishna na Wakuu wa Vitengo katika Ukumbi wa Mikutano wa Makao Makuu ya Jeshi hilo, Masauni alisema Serikali ya Awamu ya Tano kusudio lake ni kuipeleka nchi katika uchumi wa kati na viwanda hivyo ili maendeleo yapatikane lazima Jeshi hilo lijiimarishe zaidi.
“Akikisheni mna peleka maafisa wa zimamoto katika wilaya zote nchini ili wakaweze kutoa elimu kwa umma jinsi ya kuzima moto, kwasababu kinga ni bora kuliko tiba,” alisema Masauni.
Aidha, Masauni alisema zipo changamoto kadhaa zinazolikabili Jeshi hilo, ikiwemo magari ya kuzimia moto hayatoshi, vifaa vya mahokozi pamoja na ukosefu wa madawa ya kuzimia moto,  lakini Serikali itajitahidi kuzitatua kadiri ya uwezo wake.
Kwa upande wake Kamishna Jenerali wa Jeshi hilo, Thobias Andengenye, alisema amepokea maelekezo hayo kutoka kwa Naibu Waziri, na kumuhakikishia kuwa, Jeshi lake linaona ukuaji wa kasi wa viwanda nchini kunahitaji sana huduma zitolewazo na Jeshi la Zimamoto na Uokoaji.  
“Tunashukuru kwa ujio wako, maelekezo uliotupa tumeyapokea, tunakuhakikishia kujipanga zaidi katika kuongeza nguvu zaidi katika kukabiliana na majanga ya moto,” alisema Andengenye.
Hata hivyo, Andengenye aliiomba Serikali kuiongezean uwezo zaidi Jeshi hilo na kuipatia vitendea kazi vya kisasa pamoja na kuongeza rasilimali watu ili kuipa nguvu zaidi Jeshi hilo katika kutekeleza majukumu yake.
Masauni alifanya ziara hiyo ya siku moja kwa lengo la kuzungumza na viongozi wa Jeshi hilo kuhusiana na mipango ya mbalimbali ya Serikali na Jeshi hilo kuhusu kukabiliana na majanga ya moto nchini.
Mwisho/-

No comments: