Advertisements

Tuesday, October 17, 2017

MBUNGE KABATI AMETOA SH.MILIONI MOJA KWA MTANDAO WA POLISI WANAWAKE MKOANI IRINGA (TPF)

Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) akiwa sambamba na kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi
Kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi akizungumza wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF)
Kamanda wa jeshi lapolisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi  na mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati wakicheza ngoma wakati wa maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF)
Hawa ni baadhi ya  wanamtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) wakiwa katika maadhimisho ya miaka kumi toka kuanzishwa kwa mwaka 2007.

 Na Fredy Mgunda,Iringa.

Mbunge wa viti maalum mkoani Iringa kupitia chama cha mapinduzi (CCM) Ritta Kabati alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho ya miaka kumi tangu kuanzishwa kwa mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) kwa lengo la kufanya kazi kwa ukaribu na jamii.
 
Akisoma risala iliyoandaliwa na mtandao huo PC Doroth Matinde alisema kuwa mtandao wa polisi wanawake Tanzania (TPF) ulianzishwa mnamo tarehe 25 / 10 / 2007 kwa lengo la kuendelea kuifnya kazi kwa karibu kwa jamii na kufanikisha azma ya utekelezaji wa majukumu yake.

“Lakini ukiangalia na yote hayo lengo na malengo mengine ni kuunganisha askari wa kike kuwa karibu na jamii ili kudumisha mahusiano mema kati ya mtandao na wananchi hatimaye kuboresha huduma bora na kufanikisha ufanyaji kazi wetu” alisema Mtinde

Mtinde alisema kuwa mtandao huo wa polisi wanawake umekuwa ukitembelea akina mama wajane,kuwafariji na kuwapa msaada wa chakula ndani ya kambi za polisi hapa mkoani Iringa.

“Katika kuhakikisha kuwa mtandao unathamini nafasi ya mwanamke katika jamii tumekuwa mstari wa mbele kushirikiana kwa kutoa elimu ya masuala kadha kama ubakaji,ulawiti,Imani potofu na unyanyasaji wa kijinsia” alisema Mtinde

Aidha Mtinde alizitaja kazi watakazozifanya kazi katika cha maanzimisho  watafanya usafi katika maeneo ya soko kuu manispaa ya Iringa,stendi kuu pamoja na kutoa elimu kwa wanafunzi mbalimbali wa shule za msingi na sekondari ili kuzuia uhalifu na kutoa elimu ya madhara ya madawa ya kulevya na mimba za mashuleni.

Kwa upande wake mgeni rasmi Ritta Kabati aliupongeza mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) kwa kufikisha miaka kumi ya kuwatumikia wananchi na kuhakikisha wazitatua changamoto zilizowakabili wananchi na kuifanya jamii kuendelea kuishi kwa Amani.

“Kwa kweli naona wanamtandao mnajitahidi sana kufanya kazi na kazi yenu inaonekana katika jamii hasa kuanzisha hata dawati la jinsi hapa mkoani Iringa limekuwa jambo la muhimu sana kwa wanawake” alisema Kabati 

Kabati aliwachangia shilingi milioni moja kwa ajili ya kufanikisha shughli za mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) na kuhaikisha anawatafutia wafadhi wa kusaidia kutatua changamoto ili kuifikia jamii kwa urahisi Zaidi.

“Mimi natoa hiki kidogo tu lakini nitahakikisha nawatafuta wafadhili wengine ili kuendelea kuuchangania mfuko wa huu mtandao wa polisi wanawake mkoani Iringa (TPF) kwa ajili kuweza kuifikia jamii na kufanikiwa kutatua changamoto kwa haraka Zaidi” alisema Kabati

Kabati aliliomba jeshi la polisi mkoani Iringa kuhakikisha wanapeleka dawati la jinsia katika shule za msingi na sekondari ili kupunguza na kumaliza kabisa tatizo la ubakaji kwa wanafunzi kwa kuwa watakuwa wazi kuzungumza wanachofanyiwa huko mitaani.

“Tukiwa na madawati katika shule zetu itasaidia kupunguza tatizo la ubakaji kwa wanafunzi wetu hivyo kamanda naomba mtafute njia ya kuweza kufanikisha kuwa na madawati ya jinsia kama ambavyo PCCB walivyoenea katika shule mbalimbali” alisema Kabati

Naye kamanda wa polisi mkoa wa Iringa Julias Mjengi alisema kuwa jeshi la polisi hapa nchini lipo katika hatua za mwisho za kukamilisha mpango wa kulipeka dwati la jinsia kwenye shule za sekondari na shule za msingi kwa lengo lakuanza kutoa elimu mapema za ukatili wa kijisia.

“Ulicho kiongea mgeni rasmi ni kweli tatizo lipo sana mashuleni hivyo tuanza mikakati ya kuahikisha tunawafikia wanafunzi katika ngazi zote” alisema Mjengi

Mjengi alimpongeza mbunge Ritta kabati kwa juhudi zake za kulisaidia jeshi la polisi mkoani Iringa kwa hali na mali kwa kuwa amekuwa mstali wa mbele kutatua changamoto za jeshi hilo.

“Najua kuwa ulijenga kituo cha polisi kule semtema,umetoa kompyuta na mambomengine mengi ambayo jeshi la polisi tulikuwa hatuna uwezo kuyatekeleza kwa urahisi kama ambavyo kabati amefanikiwa kuyatatua” alisema Mjengi

No comments: