Meli ya Mfalme wa Oman " Fulk Al Salaam" imewasili leo Jijini Dar es Salaam kwa ziara ya siku sita inayotarajiwa kumalizika tarehe 21 Oktoba, 2017. Meli hiyo imewasili na Mjumbe Maalum wa Mfalme, Waziri wa Mafuta na Gesi wa Oman, Mhe. Dkt. Hamad Al Rumphy Mahammed ambaye ameambatana na watu zaidi ya mia tatu (300) kutoka katika sekta mbalimbali.
Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Mhe. Dkt. Hussein Mwinyi akisalimiana na Mhe. Dkt. Hamad Al Rumhy Mahammed mara baada ya kuwasili katika Bandari ya Dar es Salaam. Pembeni ya Waziri Mwinyi ni Mkuu wa Wilaya ya Kigamboni, Mhe. Hashimu Mgandila.
Naibu Waziri Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mhe. Dkt. Susan Kolimba akisalimiana na Waziri Mahammed katika sherehe za mapokezi zilizofanyika Bandarini Dar es Salaam. Pembeni yake ni Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Charles Mwijage.
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi, Dkt. Aziz Mlima akisalimiana na Mhe. Dkt. Mahammed.
Balozi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania nchini Oman, Mhe. Abdallah Kilima akisalimiana na Waziri Mahammed. Pembeni yake ni Mkuu wa Wilaya ya Temeke, Mhe. Felix Lyaniva.
Kaimu Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya Kati wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Bw. Ayoub Mndeme akisalimiana na Waziri Mahammed.
Mhe. Waziri Mwinyi akikaribishwa ndani ya Meli na Mhe. Waziri Mahammed.
Mhe. Waziri Mwinyi pamoja na Dkt. Kolimba wakiwa katika mazunguzo na Mhe. Waziri Mohammed mara baada ya kuingia ndani ya meli.
Balozi Dkt. Mlima akifatilia mazungumzo yaliyokuwa yakiendelea baina ya Mawaziri Mwinyi na Waziri Mahammed. Kushoto kwake ni Balozi wa Oman nchini, Mhe. Ali Abdullah Al-Mahruqi.
Viongozi waandamizi kutoka Serikali ya Tanzania na Oman wakijadiliana ndani ya Meli.
Vikundi vya ngoma vikitumbuiza katika viwanja vya bandari mara baada ya Meli kuwasili.
Sehemu ya watumishi wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, wakifuatilia hafla ya mapokezi ya Meli ya Mfalme wa Oman.
x
No comments:
Post a Comment