Advertisements

Wednesday, October 11, 2017

MOSHI: KIONGOZI CHADEMA APATA AJALI MBAYA YA GARI

KATIBU Mwenezi wa Baraza la Vijana wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Bavicha), Edward Simbeye amepata ajali ya gari. Simbeye alikuwa akitokea Dar es Salaam kwenda Moshi mkoani Kilimanjaro.

Akizungumza leo Jumatano asubuhi, Simbeye amesema ajali hiyo ilisababishwa na tairi la mbele kushoto kufyatuka hivyo gari kupoteza mwelekeo na kuanguka kando mwa barabara eneo la Kawawa mjini Moshi.

“Namshukuru Mungu nimetoka salama mimi na mdogo wangu… nilikuwa nakwenda nyumbani kwa sababu za kifamilia,” amesema Simbeye. GPL

No comments: