ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 11, 2017

SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA AFRICAID KUPITIA MRADI WA KISA LAWAKUTANISHA WASICHANA WA KIDATO CHA TANO NA SITA KATIKA SHULE ZA SEKONDARI ZA MKOANI KILIMANJARO.

Muwasilishaji wa mada katika kongamano lililowajumuisha Wasichana wanaosoma kidato cha tano na sita katika shule mbalimbali mkoani Kilimanjaro, Nyamagesa Laban akizungumza katika kongamano hilo lililofanyika katika Chuo cha Wanyamapori Mweka. 
Baadhi ya wanafunzi wakifuatilia kwa karibu ujumbe uliokuwa ukitolewa na Nyamagesa ambaye pia ni mwandishi wa vitabu.

Baadhi ya wananfunzi walioshiriki kongamano hilo wakiuliza maswali kwa Nyamagesa mara baada ya kumaliza kutoa ujumbe kwa wanafunzi hao.
Muwasilishaji wa mada katika kongamano la Wasichana wa Shule za Sekondari mkoni Kilimanjaro,Stumai Simba akizungumza katika kongamano hilo.
Baadhi ya wanafunzi kutoka shule mbalimbali za Mkoa wa Kilimanjaro wakifuatilia Mada zilizokuwa zikitolewa.
Baadhi ya Wanafunzi wakimuuiza maswali Muwasilishaji wa mada katika ongamano hilo.

Na Dixon Busagaga wa Globu ya Jamii, Kanda ya Kaskazini.
WASICHANA walioko shuleni wametakiwa kuacha kuchagua kazi za kufanya pindi wamalizapo masomo na badala yake wafanye maandalizi ya kujiajili kwa kufanya shughuli za ujasiliamali wakati wakiendelea na harakati za kutafuta kazi.

Mbali na hayo wasichana pia wametakiwa kujenga tabia ya kujiamini na kuacha tabia ya kuwa tegemezi ili kuondokana na mfumo uliopo katika jamii kwa sasa ya kuwa mtoto wa kike ni wa kuwezeshwa na kuhurumiwa.

Hayo yameelezwa na wawezeshaiji wakati wa kongamano lililofanyika katika Chuo cha Wanyapori (Mweka) na kuandaliwa na Shirika lisilo la Kiserikali la Africaid kupitia mradi wake wa KISA na kukutanisha zaidi ya wanafunzi 1400 kutoka shule 11 za mkoa wa Kilimanjaro .

Stumai Simba ni miongoni mwa wasichana walioamua kujiajiri na baadae wanatumika katika kutoa hamasa kwa wasichana hasa wanaojiandaa kuhitimu masomo yao ya ngazi ya sekondari kushiriki kuondoa mfumo dume katika jamii amewataka wasichana kutokata tamaa.

Msimamizi wa Mradi wa KISA mkoa wa Kilimanjaro, Devota Mlay amesema lengo la kuwakutanisha wanafunzi wa kike wanaosoma kidato cha tano na sita ni kuwaandaa kwenda kutoa elimu kwa mtoto wa kike katika jamii pindi wamalizapo masomo .

Kwa upande wa wanafunzi walioshiriki kongamano hilo wameeleza mambo wanayojifunza kupitia makongamano huku wakifurahishwa na namna ambavyo wawasilishaji wa mada walivyofanikiwa bila ya kungojea kupata ajira serikalini.

Kongamano hilo ambalo limejumisha shule za 11 kutoka wilaya za Mwanga, Rombo, Same, Siha, Hai na Moshi mjini linatarajia pia kufanyika katika mkoa wa Arusha na kuhusisha wanafunzi wa kidadto cha tatno na sita katika shule za mkoa wa Arusha.

No comments: