ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 25, 2017

RC MWANRI AZINDUA JUKWAA LA WANAWAKE WAJASIRIAMALI KALIUA

Image result for MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri
Na Mussa Mbeho , Kaliua

MKUU wa Mkoa wa Tabora Aggrey Mwanri juzi amezindua Jukwaa la Wanawake Wajasiriamali wilayani Kaliua Mkoani hapa ambalo limelenga kuwainua akinama wote kiuchumi kupitia ujasiriamali.

Akizindua Jukwaa hilo Mwanri alisema nia ya serikali ya awamu ya tano ni kuhakikisha wanake wote wanainuka kiuchumi kupitia mikakati na fursa mbalimbali zilizoainishwa katika ilani ya uchaguzi ya Chama Cha Mapinduzi.

Alisema uanzishwaji wa Jukwaa la Wanawake ni utekelezajiwa wa agizo la Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kwa kila halmashauri ili kuharakisha jitihada za kumkomboa mwanamke kiuchumi.

Alifafanua kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais John Pombe Magufuli ilishaagiza halmashauri zote kutenga asilimia 10 ya mapato yake ya ndani ya kila mwezi ili kuwezesha vikundi vya vijana, wanawake na walemavu.

Mwanri aliupongeza Uongozi wa halmashauri ya wilaya hiyo chini ya Mkurugenzi Mtendaji John Pima, Mwenyekiti wa halmashauri Haruna Kasele, Wabunge, Madiwani na Wataalamu wote kwa kutekeleza agizo hilo kwa vitendo kila mwezi.

‘Naagiza kila kikundi kitakachopewa fedha hizo kizitumie vizuri ili kuboresha biashara zao na warejeshe mikopo hiyo kwa wakati, ili wapewe wengine pia’, alisema.

Aidha aliagiza halmashauri zote kwenda kujifunza kutoka kwa wenzao wa Kaliua jinsi wanavyofanikisha zoezi la ukusanyaji mapato kwa zaidi ya asilimia 100, kuboresha utoaji huduma kwa Watendaji wa Kata na Maafisa Ugani na kutenga asilimia 10 kila mwezi kwa ajili ya wajasiriamali.

Mkuu wa wilaya hiyo Abel Busalama alisema uwepo wa Jukwaa la Wanawake katika wilaya yake utasaidia sana kuunganisha wanawake wote na kuhamasishana kujiunga katika vikundi vya uzalishaji bidhaa mbalimbali ili kuboresha maisha yao na kuchangia mapat ya serikali.

Mkurugenzi Mtendaji John Pima na Mwenyekiti wa halmashauri Haruna Kasele walisema Jukwaa hilo litakuwa chachu kubwa ya mafanikio ya wanawake katika halmashauri hiyo, waliahidi kutoa ushirikiana kwa uongozi wa Jukwaa hilo ili kufikia malengo yao.

Baadhi ya wawakilishi wa vikundi vya akinamama wajasirimali vilivyoshiriki katika uzinduzi huo vilitoka katika majimbo yote yote mawili ya Ulyankulu na Kaliua ambapo kata za Ushokora, Ulyankulu, Kaliua na Igagala ziliwakilishwa.

No comments: