ANGALIA LIVE NEWS

Wednesday, October 25, 2017

RC RUKWA AAGIZA KUFUATA UTARATIBU UINGIZWAJI WA MAHINDI KUTOKA NCHI ZA JIRANI.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen akijadiliana na Viongozi alioambatana nao akiwemo DC Kalambo Julieth Binyura  alipofanya ziara ya ghafla katika Kijiji cha Safu, kilichopo mpakani mwa Tanzania na Zambia na kujionea malori yenye shehena za mahindi yakiingizwa kiholela kutoka katika nchi ya Zambia.
 Moja ya lori lililobeba Shehena ya mahindi yaliyoinginzwa nchini kiholela kutoka katika nchi ya Zambia.
Shehena za Mahindiyaliyoingizwa  kiholela.

Mkuu wa Mkoa wa Rukwa Kamishna Mstaafu Zelote Stephen ameziagiza Halmashauri zote Mkoani kwake kuhakikisha wanakuwa na magulio rasmi ya kuuzia mahindi ili wakulima na wafanyabiashara waweze kufuata utaratibu.

Amesema kuwa kwa kufanya hivyo kutakuwa na usimamizi thabiti na taratibu za uingizwaji wa bidhaa kutoka katika nchi za jirani utafuatwa pamoja na mamlaka husika kutekeleza wajibu wake kwa mujibu wa sheria zilizopo ikiwa ni pamoja na halmashauri kupata mapato na nchi kwa ujumla.

Kauli hiyo ameitoa baada ya kufanya ziara ya ghafla katika Kijiji cha Safu, kilichopo mpakani mwa Tanzania na Zambia na kujionea malori yenye shehena za mahindi yakiingizwa kiholela kutoka katika nchi ya Zambia bila ya kuwepo kwa mamlaka husika zinazosimamia uingizwaji wa bidhaa kutoka katika nchi za jirani.

“Ni mategemeo yangu kuwa wakurugenzi wataanzisha vituo ili wakulima waweze kupeleka mazao yao hapo na kuweza kuyauza na ndipo nao halmashauri waweze kukusanya ushuru unaotakiwa, lakini hizi biashara zinazofanywa kupitia njia za panya, nasema si kitu cha kuachiwa, hivyo basi nisingependa kuona malori yanaruhusiwa kwenda maeneo ambayo siyo mipaka rasmi kuchukua mizigo na kuingiza nchini,” Amesema.

Na kuongeza kuwa hakuna tatizo kufanya biashara na nchi za jirani isipokuwa biashara hizo zifanywe kihalali kwa kufuata sheria zilizowekwa.
Halikadhalika Mh. Zelote Alisema kuwa Mkoa wa Rukwa una mahindi ya kutosha na wafanyabiashara wa mikoa mingine wafike kununua na sio kuvuka mipaka kwa njia za kupanya kufanya biashara hiyo.

Kwa upande wao wafanyabiashara waliohojiwa na Mh. Zelote katika ziara yake hiyo walidai kuwa mahindi yanayotoka Zambia bei yake ni nafuu zaidi kuliko ya Tanzania lakini pia wakulima wa Tanzania huficha mahindi yao wakisubiri kupanda kwa bei jambo ambalo ni hasara kwa wafanyabiashara wanaotoka nje ya Mkoa wa Rukwa.

“Wakulima wa Mkoa wa Rukwa huficha mazao yao wakisubiri kupanda kwa bei, sasa kama mimi mfanyabiashar natokea Mwanza nakuja kwa mahesabu ya kuchukua mzigo na kuondoka, nikisema nimsubiri huyu mkulima aliyeficha mazao yake hadi yaapande mimi nakula hasara,” Amiri Giti mfanyabiashara kutoka Mwanza alisema.

No comments: