Advertisements

Saturday, October 21, 2017

SHINE WITH SHINA 15TH ANNUAL FUNDRAIZER 2017 GREENBELT, MARYLAND YAFANA

Shine na SHINA 15th Annual Fundraiser iliyofanyika Hilton Inn Greenbelt, Maryland nchini Marekani siku ya Ijumaa Oktoba 20, 2017 na kuhudhuliwa na wadau mbalimbali wanayoiunga mkono SHINA.

Katika Fundraiser hiyo pia ilifanyika bahati nasibu ya tiketi ya ndege ya kwenda Tanzania  na kurudi Marekani ambayo mshindi wake alikua Bernadeta Kaiza.

Pia vitu mbalimbali viliuzwa kwa ajili ya kuchangia jamii wasiojiweza wenye wasiokuwa na uwezo hata kununulia nguo na viatu watoto wao wakiwemo kusaidia watoto wenye ulemavu ambao ndoto yao ni kupata elimu ya msingi mpaka ya chuo kikuu.
Mchungaji Francis Forsang akifungua  Shine with SHINA 15th Annual Fundriser kwa sala siku ya Ijumaa Oktoba 20, 2017 iliyofanyika katika hotel ya Hilton Inn Greenbelt, Mryland na kuhudhuriwa na wadau mbalimbali wanje na ndani ya Marekani. Picha naVijimambo Blog na Kwanza Production
Rose Woodruff ambaye ni VP Community Outreach akifungua Shine with SHINA 15th Annual Fundriser kwa kuelezea jinsi anavyofanya kazi kwa karibu nao na jisni alivyokwenda Tanzania kujionea mwenyewe kazi kubwa ya SHINA waifanyao kusaidia jamii zisizokuwa na kipato katika sehemu mbalimbali za Tanzania.
Amos Mushala akielezea mafanikia na changamoto za SHINA tangu kuanzishwa kwake miaka 15 iliyopita.
Amos Mushala akimkaribisha CEO wa SHINA Bi. Jessica Mushala ambaye ni mke wake kuja kudadavua mawili matatu kwenye sehemu mbalimbali kwa kazi kubwa wanayofanya kusaidia jamii Tanzania hasa kwenye familia zisizokua na kipato.
Wakina mama wakijimwaga uwanjani na kumsindikiza Bi. Jessica Mushala kabla ya kuongea,
Bi. Jessica Mushala akiongea na wadau mbalimbali waliofika kwenye Shine with SHINA 15th Annual Fundriser siku ya Ijumaa Oktoba 20, 2017 iliyofanyika katika hotel ya Hilton Inn Greenbelt, Mryland 
Bi. Jessica Mushala akimzawadia moja ya wadau wanaoiunga mkono SHINA kwa hali na mali.
Ms April Richardson ambaye ni President/(CEO) Opportunity LLC akiongea kama mgeni rasmi wa Shine with SHINA 15th Annual Fundriser siku ya Ijumaa Oktoba 20, 2017 iliyofanyika katika hotel ya Hilton Inn Greenbelt, Mryland 
Patrick Omondi na mkewe mama Bertha kutoka Kenya wanaojishughulisha na shughuli za kusaidia jamii kama wafanyavyo SHINA akielezea na kuishukuru SHINA kwa mwaliko wao kuja kujifunza wanachofanya na kwamba wapo tayari kufanya kazi pamoja.
KWA PICHA ZAIDI BOFYA SOMA ZAIDI

Francis Richards akitoa burudani na ngoma ya pipa.
Juu na chini ni msanii Anna Mwalago akiimba moja ya nyimbo zake.
Mshereheshaji Tuma akionyesha tiketi ya ndege ambazo tiketi zake za baati nasibu zilinunuliwa kwa $10.
Mshindi wa bahati nasibu Bernadeta Kaiza akifurahia kushinda kwake tiketi ya ndege.
Bi. Jessica Mushala akimwelekeza jambo Tuma.
No comments: